Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) imeunga mkono pendekezo la kusimamis
ha mapigano katika mji wa Aleppo huko Syria.
Pablo Marco, Mkurugenzi wa jumuiya hiyo katika eneo la
Mashariki ya Kati amesema kuwa MSF inakaribisha hatua ya Russia ya
kuunga mkono suala la kusimamisha vita kwa muda wa masaa 48 katika mji
wa Aleppo nchini Syria. Marco ameongeza kuwa wakazi wa Aleppo
wanahitajia sana amani na utulivu.
Mkurugenzi wa Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) amesema
usitishaji vita kwa muda wa masaa 48 huko Aleppo utatoa fursa ya
kupelekwa misaada katika mji huo na kuwaondoa raia waliojeruhiwa na
wagonjwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Wizara ya Ulinzi ya Russia jana ilitangaza kuwa inaunga mkono
pendekezo la Stephen de Mistura, Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa
katika masuala ya Syria la kusimamisha mapigano huko Aleppo kwa muda wa
saa 48.
Wizara hiyo imesema pia kuwa Moscow ipo tayari kusaidia utekelezaji
wa makubaliano hayo wiki ijayo. Jeshi la Syria likisaidiwa na vikosi
vya jeshi la anga la Russia tangu wiki mbili zilizopita lilianzisha
oparesheni kubwa ya kijeshi kwa minajili ya kuwatimua magaidi katika mji
wa Aleppo na hadi sasa magaidi wa Daesh na wa makundi mengine ya
kigaidi zaidi ya 1000 wameuliwa na wengine karibu 2500 kujeruhiwa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269