Wajumbe na Viongozi wa Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi wakiwa kwenye picha ya pamoja
baada ya kushiriki Semina ya Uhamasishaji wa Ujenzi wa Masjala za Ardhi zaVijiji,
Kukabidhi Mpango wa matumizi Bora ya Ardhi wa Wilaya na kutambulisha timu ya upimaji
Mipaka iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro.
Na Salum Mwinyimkuu, Morogoro
Zaidi ya hatimiliki 300,000 za Ardhi zinatarajiwa kutolewa kwenye Wilaya za KILOMBERO, MALINYI na ULANGA mkoani Morogoro kupitia mradi wa kuwezesha Urasimishaji Ardhi wa LTSP, ili kupunguza Migogoro ya Mipaka kwenye Vijiji.
Miongoni mwa Changamoto inayofifiza Juhudi za Serikali kumaliza tatizo la Migogoro ya Ardhi katika Wilaya za KILOMBERO, MALINYI na ULANGA ni Rushwa kwa Baadhi ya Watendaji wasio waaminifu.
Wilaya ya KILOMBERO yenye vijiji 99 imejizolea Umaarufu kwa kuwa na maeneo mengi yenye Utata wa Ardhi,ikihusisha migogoro ya Mipaka baina ya kijiji na kijiji, hifadhi na kijiji pamoja na wakulima na wafugaji.
Ili kuhakikisha Changamoto hiyo inabaki Historia, mradi wa kuwezesha Urasimishaji Ardhi umetua Wilayani Kilombero, ukiwa na Shabaha ya kupima mipaka ya Vijiji 20,na kupatiwa Hatimiliki ya Ardhi ili kuondoa Migogoro hiyo.
MARY MAKONDO ni Kaimu kamishna wa Ardhi nchini akizungumza Wilayani humo, ameeleza umuhimu wa Mradi huo unaofadhiliwa kwa Dola Milioni 15.2, wenye lengo la Kurasimisha Ardhi ili imnufaishe Mwananchi wa Masikini na kuondoa Migogoro isiyo na tija.
Zoezi hilo la Urasimishaji Ardhi na Utoaji wa Hatimiliki za Kimila litaenda sambamba na Ujenzi wa Masjala za Ardhi kwenye Vijiji vilivyopo kwenye mpango wa LTSP,lengo likiwa ni kuweka sawa kumbukumbu za Mikataba inayohusu Ardhi.
Itakumbukwa Mradi huu ni matokeo ya Mkutano wa wakuu wa nchi zenye Uchumi Mkubwa Duniani, ambapo Tanzania ilialikwa kuhudhuria kama mshiriki, ambako kulizinduliwa Ushirikiano kati yake na Kundi la G8 kuhusu uwazi kwenye sekta ya ardhi.
|
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269