Jose Eduardo dos Santos amekuwa madarakani kwa miaka 36
Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos aliyeongoza kwa miaka 36 amechaguliwa tena kuwa kiongozi wa chama tawala cha MPLA.
Uchaguzi wa bunge unatarajiwa kufanywa mwaka ujao, na kiongozi wa chama kinachoshinda ndiye anayekuwa rais.
Rais dos
Santos alisema awali mwaka huu, kwamba ataondoka madarakani mwaka wa
2018, lakini ameshawahi kutoa ahadi kama hizo kabla.
Kiongozi
huyo mwenye umri wa miaka 73, analaumiwa kuwa amekusanya madaraka mengi
na mali, kwenye mikono ya familia yake na washirika wake wakubwa
kisiasa. BBC
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269