Na
Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Halmashauri
ya Manispaa ya Temeke imeandaa
operesheni kabambe katika stendi ya Mbagala ili kuhakikisha biashara zote zinafanyika
katika maeneo yaliyotengwa na yasiyohatarisha afya ya jamii.
Hatua
hiyo imefikiwa baada ya kuongezeka kwa malalamiko kutoka kwa wananchi wa eneo
hilo juu ya wafanyabiashara mbalimbali waliovamia eneo hilo na kulifanya kuwa
la biashara.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Halmashauri
hiyo, Nassib Mbaga na kuwataka wafanyabiashara wanaofanya biashara zao katika
mazingira yasiyo rasmi kuacha mara moja kwani ni kinyume cha sheria na
taratibu.
“Tumeandaa operesheni kabambe ya kuondoa Kero zilizogundulika katika
stendi ya Mbagala ili kuhakikisha kwamba biashara zote zinafanyika katika
maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli hizo” alisema Mbaga.
Aliongeza kwa kuwataka watu wote wanaofanya biashara bila kibali katika
maeneo ya stendi hiyo waondoke kabla ya zoezi la kusafisha halijaanza na kwa
wale watakaokaidi, hatua za kisheria zitachukulia dhidi yao.
Aidha Mbaga alieleza kuwa kumekuwepo na jitihada za wazi za kuiweka
Halmashauri katika hali ya usafi ikiwemo kutoa elimu kwa umma pamoja na kuhamasisha
wananchi kuweka mazingira katika hali ya usafi na kuzuia unywaji wa maji ya
kwenye vifuko vya plastiki yajulikanayo kama viroba/Kandoro kwa kuwa hayana viwango vya ubora.
Vilevile Halmashauri hiyo itaendelea kuwakamata wale wote wanaofanya
biashara hiyo na kuteketeza mali zao kisha kuwafikisha Mahakamani au kuwalipisha
faini.
Mkurugenzi huyo ameyataja maeneo matano ambayo yametengwa rasmi kwa ajili
ya biashara yakiwemo soko la Toangoma, Kilamba, Makangarawe, Sigara na Kiponza
ambapo maeneo hayo yana huduma zote za jamii ikiwemo vyoo bora.
Maeneo mengine yaliyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya Masoko ni
pamoja na Temeke Stereo, Vetenari Tazara, Madenge, Tandika Kuu, Tandika
Kampochea, Keko Magurumbasi, Temeke Mwisho, Bulyaga, Kizuiani, Zakhem, Mbagala
Rangi tatu, Kampochea Mbagala, Mtoni Mtongani, Lumo, Urassa,Feri, Maguruwe,
Limboa na Kabuma.
Mkurugenzi Mbaga ametoa rai kwa wananchi wanaohitaji kupata nafasi za
kufanyia biashara katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo kufanya
mawasiliano na Ofisi yake ili kupatiwa maeneo rasmi kwa ajili ya shughuli hizo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269