Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum
Na Sheila Simba-MAELEZO
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ametoa wito kwa viongozi wakisiasa Nchini, kuwa wavumilivu ili kulinda Amani ya Nchi.
Sheikh Alhad ameyasema hayo leo, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam ambapo amewataka viongozi hao kutii mamlaka iliyoko kwani mamlaka hiyo imewekwa na Mungu na hivyo ni vema kutafuta njia nyingine kumaliza matatizo yanapotokea.
“Ipo haja ya kuvumiliana kwa ajili ya Taifa letu, kwani yanapotokea machafuko waathirika wakubwa ni wanawake, watoto na vijana wetu ambao wanaweza kupata madhara makubwa na hata kupoteza maisha’’alisema Alhad
Akizungumzia maandamano ya ukuta yaliyopangwa kufanyika Septemba Mosi, amesema kuwa kauli ya kuzuia
maandamano hayo imetolewa na Rais wa Nchi na kuomba kauli hiyo kuchuliwa kwa uzito wa kipekee, kwani busara ni kusikiliza mamlaka imesema nini na kutii kauli hiyo ya Rais.
maandamano hayo imetolewa na Rais wa Nchi na kuomba kauli hiyo kuchuliwa kwa uzito wa kipekee, kwani busara ni kusikiliza mamlaka imesema nini na kutii kauli hiyo ya Rais.
“Nawashauri Watanzania wenzangu, viongozi wangu wa kisiasa jambo hilo si vyema tukashiriki kwani kutotii mamlaka ni dhambi ndivyo vitabu vya dini vinanavyosema,’’ alifafanua Sheikh Alhad
Ameongeza kuwa suala la kulinda amani ni la watanzania wenyewe kwa kusaidiana na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha amani inaendelea kuwepo, kwani ni rahisi kupoteza amani tuliyonayo lakini ni vigumu kurudisha amani.
Amesema kuwa vijana wasikubali kutumika kwa maslahi ya watu wengine kwani kufanya hivyo ni kushindana na dola na kutolea mfano wa machafuko yanayoendelea kwa baadhi ya Nchi Duniani na kupelekea mataifa hayo kutokalika kutokana na vurungu za kisiasa.
Aidha amewaomba vijana kutokubali kulitia doa Taifa, kwani Tanzania inafahamika ni kisiwa cha Amani Duniani na inapaswa kulinda heshima hiyo ili kuendelea kutunza amani ya Watanzania wote bila kujali tofauti za kisiasa.
Amewaomba viongozi hao wa kisiasa kuwasilisha malalamiko yao kwa njia tofauti kwani Serikali iliyopo madarakani ni sikivu na ipo kwa ajili ya wananchi wote.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269