Mkuu wa
Idara ya Fedha na Utawala wa Benki ya Maendeleo, Peter Tarimo akisaini
mkataba wa udhamini wa shindano la Gospel Star Search (katikati) huku
meneja wa Mrado huo wa GSS, Samwel Sasali (kushoto) akishuhudia tukio
hilo lililofanyika jana hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam.
Siku ya
jana Kamati Ya Gospel Star Search na Kampuni mbili ambazo ni Maendeleo
Bank na Grace Product Wametiliana Mkataba wa Udhamini wa Gospel Star
Search 2016. Pichani tukio likifanyika Regency Hotel. Milango ipo wa
Wadhamini wengine Pia Makampuni na watu Wa Mavazi Mnakaribishwa.
Meza kuu.
Ndugu
waandishi wa habari tunashukuru sana kwa kuitikia wito wetu siu ya leo,
katika project hii kubwa inayoendelea ya Gospel star search. Tulikwisha
kuanza toka na tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa mpaka sasa lakini lengo
kuu hasa la uwepo wetu hapa siku ya leo ni kuwajuza juu ya uwepo na
kutiliana saini na wadhamini wetu ambao wameona ni vyema na
tumekubaliana kufanya kazi pamoja katika project hii ya Gospel star
search. Nitamkaribisha mwenzangu yeye atasema zaidi kuhusu GSS na hatua
tuliofikia mpaka sasa na kuwatambulisha wadhamini wetu.
LENGO KUU
Ahsanteni sana waandishi wa habari kwa kuitikia wito wetu, kama
alivyosema mwenzangu lengo letu siku ya leo ni kuwatambulisha wadhamini
wetu kwenu na kwa watanzania ,lakini kabla ya kwenda mbali ni
vyematukatoa mrejesho mfupi juu ya GSS ilipoanza mpaka hatua tuliofikia
kwa mwaka huu.
GSS ina
lengo kubwa ya kutafuta waimbaji wa muzii wa injili na kuwasaidia
kujitambua kuwapa nafasi ili kukuza vipaji vyao na kuvifanya vionejkane
kwa watu kwaajili ya kua faida kw watu lakini hata kwao wenyewe
pia.Tunaamini sana kipaji kama kikitumika kwa namna ilio sawa kinaweza
kubadili kabisa maisha ya mtu na akawa mtu mwingine mwenye maisha bora
yalioletwa na kipaji au talanta alionayo hii ndio sababu tumeipa kauli
mbiu ya KIPAJI CHAKO…
HATMA
YAKO. Tumeanza na wilaya tatu za mkoa wa Dar es salam kwa sasa,
Kinondoni, Temeke pamoja na Ilala na kila sehemu tumechua washiriki wa
tano hivyo kua na jumla ya wshiriki 15 kwa wilaya zote 3 ambao hawa ndio
wamefanikiwa kuingia hatua ya nuusu fainali. Mchakato wetu umekua na
round mbili (2) za mchujo ambazo kwazo ndizo zimetupa washiriki hawa 15
waliopo mpaka hivi sasa.
Ndugu
waandishi wa habari tunashukuru sana wadhamini wetu ambao waliona ni
vyeama kushiriki na sisi kwa kutufanyia udhamini kwenye project hii
kubwa ya GSS, ambao leo tuko nao hapa kwaajili ya kuwatambulisha rasmi
kwenu..ambao ni • Maendeleo Bank • Grace Product • Brand exponetial
• Kiango
media • Clouds Media Group • Fm studios (Faith music lab) • 3D Kwa hiyo
uwepo wetu hapa ni kuwatambulisha rasmi watu hawa amabao wameona ni
vyema kusimama na sisi na pia kutiliana saini mbele yenu kama ishara ya
kuingia ubia katika project GSS. Kwa kusema haya sasa nitatoa nafasi kwa
wadhamini kusema kdogo ju yao lakini pia juu ya GSS karibuni sana!
HITIMISHO
Pia tungependa kuchukua fulsa hii kutoa wito na hamasa kwa makampuni
mengine ambao wanaweza kushirikiana na sisi kama wadhamini kweye project
hii ya GSS bado milango ipo wazi na tutafurahi sana kushirikiana na
ninyi katika project GSS 2016 ,Uwanja wetu ni mpana na jukwaa letu ni
kubwa hivyo itakua ni nafasi ya manufaa kwetu na kwenu pia kama mtaamua
kutuunga mkono nkwa udhamibni katika project hii ya GSS 2016 kwa hatua
zilizosalia za nusu fainali na fainali. Baada ya kusema haya ninaomba
niwashukuru tena kwa uwepo wenu na hayo ndio yalikua maelezo juu ya lile
lililotuweka hapa siku ya leo. (P.T)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269