Wiki
mbili baada ya kushindwa katika uchaguzi wa jimbo la Mecklenburg
Vorpommern, Chama cha Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, cha CDU
kimeshindwa vibaya kwa mara nyingine katika uchaguzi wa jimbo la Berlin.
Sababu
kuu ya chama hicho kupoteza nguvu katika uchaguzi huo wa Jumapili, ni
sera ya Merkel ya kukaribisha wahamiaji. Matokeo ya jana ya chama cha
CDU ni mabaya kuwahi kutokea katika jiji la Berlin, na yanamuongezea
shinikizo kansela Merkel kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Chama cha
CDU kimepata asilimi 17.5 ya kura zote, na kimepoteza asilimi 5.8 ya
kura ikilinganishwa na uchaguzi uliopita. Huku chama mshirika cha Meya
wa Berlin, Michael Müller, kinachofuata siasa za wastani za mrengo wa
kushoto cha SPD kikishinda asilimia 21.6 ya kura zote zilizopigwa,
kikiwa kimeanguka kwa asilimi 6.7 ikilinganishwa na uchaguzi uliopita wa
jimbo hilo.
Licha ya kupungua kwa uungwaji mkono wa chama chake, Meya Müller amesema chama cha SPD kimefikia lengo lake.
"Tumefikia
lengo letu, bado tunasimama kama chama kilicho na nguvu zaidi katika
mji huu na tuna mamlaka ya serikali. Tumewazidi washindani wetu wa
asilimia 5, 6, 7.
Tumefanikiwa kupata matokeo yanayo tuwezesha kuenedelea kushikilia nafasi ya umeya," amesema Müller.
Tumefanikiwa kupata matokeo yanayo tuwezesha kuenedelea kushikilia nafasi ya umeya," amesema Müller.
Chama cha AfD kimeongeza uungwaji mkono.
Wakati
huo huo, chama cha mrengo wa kushoto kilichokuwa chama cha kikomunisti
cha iliyokuwa Ujerumani ya Mashariki, kimejiongezea asilimi 4 ya kura na
kupata asilimi 15.7. Huku chama kipya cha siasa kali za mrengo wa kulia
cha AfD kikishinda asilimia 14.1 ya kura zote zilizopigwa, na
kujinyakuli kiti cha kumi katika uchaguzi wa majimbo.
Asilimia
66.6 ya watu walijitokeza kupiga kura, idadi hii ikiwa imeongezeka
ikilinganishwa na asilimi 60.2 ya uchaguzi uliopita. Chama cha AfD
kilifanikiwa kuvutia wapiga kura wapya, lakini pia kimeweza kunyakuwa
baadhi ya wafuasi wa vyama vya CDU na SPD pamoja na vyama vingine.
Georg
Pazderski, mgombea wa chama mbadala kwa Ujerumani cha AfD amekisifu
chama chake kwa namna kilivyoweza kupiga hatua katika muda mfupi tokea
kuasisiwa kwake.
"Kutoka
sifuri hadi tarakimu mbili, ni jambo la namna ya pekee kabisa mjini
Berlin, halikuwahi kutokea kwa miaka 66. Na matokeo yanasemaje? Muungano
mkuu umepoteza kura.... Bado huajapoteza kura katika kiwango cha
shirikisho lakini hilo linakuja nalo mwakani," amesema Georg Pazderski.
Ingawa
vyama vya Social Democratic SPD na Cristian Democratic Union CDU
vimeibuka kuwa na nguvu zaidi katika uchaguzi wa jimbo la Berlin
uliofanyika jana, lakini pia vimetoteza uungwaji mkono mkubwa kiasi ya
kwamba havitaweza kuendelea kuongoza serikali ya muungano ya Ujerumani.
Katibu
Mkuu wa chama cha CDU, Peter Tauber, ameulamu uongozi wa meya wa Berlin
Müller wa muungano wa vyama vya SPD na CDU, kwa matokeo yasiyoridhisha
ya chama chake cha CDU. DW
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269