GERSON MSIGWA |
DAR ES SALAAM
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imewatahadharisha wananchi kuwa kuna watu wametumia nembo ya kurugenzi hiyo na jina la Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, na kuchapisha kisha kusambaza kwa barua kwa kampuni binafsi na Wakurugenzi Watendaji wa wakiwataka kuchangia fedha kwa ajili ya kinachodaiwa kuwa rekebisho la Bajeti za miundombinu na mfuko wa Maendeleo ya Jamii utakaofanyika katika kumbi za Bunge mjini Dodoma, Septemba 21, mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Msigwa, imesema, barua hiyo kuhusu mkutano huo, haijaandikwa na Ofisi yake hivyo siyo ya kweli.
Ifuatayo ni Tarifa kamili kutoka Ikulu
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kuwatahadharisha kuwa kuna watu
wametumia nembo ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na jina la Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu kuchapisha na kusambaza barua kwa Kampuni Binafsi
na Wakurugenzi Watendaji wakiwataka kuchangia fedha kwa ajili ya kile
kinachodaiwa kuwa ni "Mkutano Mkuu
wa Rekebisho la Bajeti za Miundombinu na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
utakaofanyika katika kumbi za Bunge Dodoma kuanzia tarehe 21/09/2016 hadi
23/09/2016"
Mnataarifiwa
kuwa barua hizo zilizotiwa saini na muhuri wa kughushi na ambazo hata maelezo
yake hayaeleweki vizuri hazijaandikwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu
na kwa maana hiyo zimeandikwa na watu wenye nia mbaya na wanaolenga kujipatia
fedha kwa utapeli.
Yeyote
aliyepokea barua hizo azipuuze na achukue hatua mara moja kwa kutoa taarifa
katika vyombo vya dola kwa kuwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu
haijaandika barua hizo na haitambui Mkutano huo.
Aidha,
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kuueleza umma kuwa uendelee
kupokea taarifa sahihi zinazotolewa kupitia vyombo vya habari na pale ambapo
kuna mashaka juu ya taarifa zenye nembo ya Ikulu wasisite kuwasiliana moja kwa
moja kwa njia ya simu zilizotajwa katika anuani ya mawasiliano hapo juu.
Tafadhari
atakayepata ujumbe huu umtaarifu na mwenzake.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar
es Salaam
17
Septemba, 2016
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269