Na Mwandishi Maalum, New York
Viongozi
Wakuu wa Nchi na Serikali, jana ( jumatatu) wamepitish tamko la kwanza la
aina yake linalolenga pamoja na mambo
mengine kuichagiza jumuiya ya kimataifa
kushirikiana katika kukabili wimbi
kubwa la wakimbizi na wahamiaji.
Kupitia
Tamko hilo ambalo linatambulika
kama Tamko la New York, linazitaka
serikali za mataifa yote, bila kuingilia
uhuru wa mambo yao kama mataifa huru au
ukiukwaji wa sheria za kimataifa, kuwapokea, kuwahifadhi na kuwapatia
huduma za kijamii wakimbizi na wahamiaji
bila ya kujali hadhi zao.
Ni tamko ambalo
limetokana na majadiliano ya muda mrefu baina ya nchi wanachama wa Umoja
wa Mataifa, Asasi za kiraia na Mashirika
ya Kimataifa, majadiliano ambayo wakati
mwingine ililazimu wajumbe kukubaliana kutokukubaliana katika baadhi ya vipengele vya tamko hilo.
Upitishwaji wa Tamko hilo la New York kuhusu
wakimbizi na wahamiaji umefanyika ikiwa na sehemu ya uliokuwa mkutano wa siku moja
uliojadili changamoto kuhusu wakimbizi
na wahamiaji ambao idadi yao imezidi kuongeza na kubwa kuwahi kutokea.
Kwa
mfano, takwimu zinaoonyesha kwamba, mwaka 2015 idadi ya wakimbizi na wahamiaji
ilifikia watu milioni 224, ongezeko ambalo kasi yake ni kubwa kuliko ongezeko
la idadi ya watu duniani.
Hata
hivyo inaelezwa pia kwamba kuna
takribani watu 65 milioni ambao wamelazimishwa kuhama,
wakiwamo zaidi ya wakimbizi milioni 21, milioni tatu wanaotafuta hifadhi na zaidi ya milioni 40
wakiwa ni wakimbizi wa ndani.
Wakuu
wa Nchi na Serikali pamoja na wakuu wa
Mashirika na Taasisi za
Kimataifa, wanaahidi kupitia
tamko hilo la New York , pamoja na mambo mengine, kulinda haki za binadamu
za wakimbizi na wahamiaji wote
bila ya kujali hadhi yao. Ikiwa ni pamoja na haki za wanawake na wasichana
pamoja na kukuza fursa yao ya kushiriki kikamilifu katika kutafuta suluhu.
Wameahidi
pia kuzuia vitendo vya ukatili wa
kingono na udhalilishaji dhidi ya wanawake. kuhakikisha kwamba watoto wakimbizi
na wahamiaji wanapata elimu mara tu wanapofika nchi ya ugenini.
Vile
vile tamko hilo, linashauri na
kupendekeza nchi ambazo zimekuwa ama zikipokea wakimbizi na kuwahifadhi au zile ambazo ni njia
wanayopitia kwenda nchi nyingine basi zisaidiwe katika ubebaji
wa jukumu hilo.
Tamko
hilo pia linataka kukomeshwa kwa tabia
ya kuwaweka vizuizini watoto ili kubaini
hadhi yao ya uhamiaji. Linataka pia kutafutiwa makazi wakimbizi wote ambao
wanatambuliwa na Kamisheni ya Umoja wa
Mataifa kuhusu wakimbizi kuwa wanaohitaji makazi, pamoja na kuwatafutia fursa za kuhamia nchi nyingine.
Wakati
huo huo, Rais wa Marekani, Barack Obama,
ameeitisha siku ya jumatano Mkutano wa Viongozi kuhusu Wakimbizi. ( Leaders’ Summit on Refugees) . Katika mkutano huo viongozi wakuu wa nchi na serikali
walioalikwa watatarajiwa kutoa ahadi zao kuhusu namna serikali zao
zitakavyo wasaidia wakimbizi.
Tanzania
ni kati ya nchi zilizoalikwa kuhudhuria
na kushiriki mkutano huo. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Augustin Mahiga ( Mb)
anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika
Mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa. Anatarajiwa kuwasilisha ahadi ya
Tanzania katika Mkutano huo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269