Breaking News

Your Ad Spot

Sep 29, 2016

PUMA YAZINDUA HUDUMA MPYA YA UNUNUZI WA MAFUTA KWA KUTUMIA AIRTEL MONEY


 Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Suni Colaso wakiliana saini mkataba wakati wa  uzinduzi wa huduma mpya inayojulikana kwa jina la Airtel Money Tap Tap Gusa Usepe inayomuwezesha mteja wao kununua mafuta kwa kutumia kadi ya Airtel badala ya kutoa fedha taslimu.

 Gari la mteja likiwekewa mafuta baada ya kununua kwa kutumia Airtel Money katika Kituo cha mafuta cha Puma Oysterbay Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Suni Colaso na Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti.

 Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti (kushoto) akibadilishana hati za makubaliano na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Suni Colaso

  Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Suni Colaso wakionesha kadi za airtel zinazotumika kununulia mafuta



 Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni za Puma na Airtel wakiwa katika hafla hiyo.

 Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti akihutubia wakati wa hafla hiyo.

  Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti akihutubia wakati wa hafla hiyo.



 Baadhi ya wafanyakazi wa Puma, Airtel na wanahabari wakiwa katika hafla hiyo







 Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Suni Colaso wakipongezana baada uzinduzi

Kituo cha mafuta cha Puma Oysterbay



MENEJA Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti amesema wanalo jukumu la kuhakikisha huduma wanazitoa kwa ajili ya Watanzania zinakuwa salama wakati wote ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuhamasisha kutumia njia za kieletroniki kwenye malipo ya fedha.



Kauli hiyo alitoa Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa huduma mpya inayojulikana kwa jina la Airtel Money Tap Tap ambayo inamuwezesha mteja wao anapotaka kununua mafuta kwa kutumia kadi ya Airtel badala ya kutoa fedha taslimu akiwa kituo cha mafuta.



Alisema wanaamini kuwa wanawajibu wa kufanya huduma zao kwa usalama, senye ufanisi na rahisi zaidi kwa wateja wao na kufafanua ni hatari kubeba fedha wakati wote maana ni rahisi kuhatarisha maisha.



Corsaletti alisema ili kufanya jamii ya Watanzania inakuwa salama wakati wote imeona kuna haja ya kuwa na huduma hiyo ambayo itamuwezesha anayehitaji kununua mafuta kwenye vituo vya Puma vilivyopo maeneo mbalimbali ya Dar es salaam wanatumia kadi za Airtel kununua mafuta.



"Milango yetu iko wazi kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma zetu na kuna jambo lolote ambalo tunaweza kulifanya ili jamii yetu  kuwa salama wakati wote.Hivyo kuna umuhimu wa kuwa na matumizi ya kadi ya Airtel katika kununua mafuta kwenye vituo vyetu vya Puma,"alisema.



Corsaletti alisema chini ya utaratibu huo mtu yeyote aliyejisajili na huduma ya Airtel Money atakuwa na uwezo wa kulipia bidhaa za Puma katika vituo vyake vyote nchini kwa kutumia kadi  ya huduma ya Airtel Tap Tap  badala ya kutumia fedha kwa ajili ya huduma kama hizo.



"Kadi hii imeundwa kwa namna ambayo wakati wa kutumika kufanya malipo , hupunguza fedha kwa kiasi cha malipo kutoka katika akaunti ya Airtel Money ya mnunuzi kwenda kwenye akaunti  ya muuzaji.



"Kadi hii itakuwa inauzwa kwa bei ya Sh 2, 000 kwenye vituo vyote vya Puma Dar es Salaam na maduka yote ya Airtel Tanzania,"alisema.



Hata hivyo alisema kuwa Kuanzia mwakani kadi hizo zitakuwa zinapatikana katika vituo vyote vya mikoani ambavyo vipo chini ya Puma.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Suni Colaso alisema wamefurai kuazisha njia hiyo ya malipo kwa kushirikiana na kampuni hiyo.



Alisema ushirikiano huo utaongeza ufanisi na kubadilisha maisha ya jamii kwa ubora zaidi kwa watanzania katika kuendelea kupata huduma muhimu kwa urahisi kupitia kadi zao za Tap Tap.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages