Mtoto
Juma Ramadhan mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi ya
Tabata Kimanga, akiwa amembeba mdogo wake Sara Sadiki wakati wakipita
katika daraja la miti linalounganisha wakazi wa Tabata Kimanga na Tabata
Chang'ombe Dar es Salaam , ambapo wakazi wa eneo hilo wanaiomba
Manispaa ya Ilala iwajengee daraja la kudumu.
Mjumbe
wa Serikali ya Mtaa wa Amani, Jonathan Mlay akimuonesha mwandishi wa
mtandao huu, daraja la miti wanalolitumia lililojengwa kwa nguvu za
wananchi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hiyo.
Na Dotto Mwaibale
WANANCHI
wanaoishi mpakani mwa Tabata Kimanga na Chang'ombe katika Manispaa ya
Ilala jijini Dar es Salaam wameomba kujengewa daraja ili waweze kutumia
muda mfupi wa kufika katika maeneo hayo badala ya kupitia Tataba
Mawenzi.
Ombi hilo wamelitowa Dar es Salaam jana wakati wakizungumza na mtandao wa www.habari za jamii.com kuhusu changamoto mbalimbali zilizopo katika eneo hilo ikiwemo ya kujengewa daraja hilo lililopo Mtaa wa Amani.
Akizungumzia
changamoto ya daraja hilo, mkazi wa eneo hilo Tusekelege Ambonisye
alisema wamekuwa wakitumia muda mwingi wa kuzunguka na gari kupitia
Tabata Bima na kwenda Tabata Chang'ombe lakini kama daraja hilo
linalounganisha maeneo hayo lingejengwa lingewarahisishia" alisema
Ambonisye.
Aliongeza
kuwa adha kubwa waliyonayo ni pale ikinyesha mvua kwani maji yanajaa na
barabara hiyo kushindwa kupitika ikiwa ni pamoja na kuhatarisha maisha
ya watu wanaojaribu kupita kaika eneo hilo.
Alisema
kutokana na adha waliyokuwa wakiipata wananchi wa eneo hilo walikusanya
nguvu na kujenga daraja la miti la muda ambalo linatumika lakini sio
salama kwa watumiaji.
Mjumbe
wa Serikali ya Mtaa huo wa Amani, Jonathan Mlay alisema changamoto ya
daraja hilo ni ya muda mrefu kwani waliwahi kuiwasilisha kwa wabunge wa
jimbo hilo waliopita na wa sasa Bonah Kaluwa lakini bado halijapatiwa
ufumbuzi wowote.
"Kupitia
vikao vyetu vya kamati ya maendeleo ya mtaa changamoto hii tuliipeleka
kwa wabunge waliopita pamoja na huyu wa sasa tupo tunasubiri matokea
yake" alisema Mlay.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269