Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh, Ummy Mwalimu akipiga ngoma ya asili wakati wa
madhimisho ya siku ya wazee duniani yaliyofanyika kitaifa wilaya ya
mbalali, mbeya 1.10.2106
Wazee
wakipita mbele ya mgeni rasmi Mh. Ummy Mwalimu wakati wa kilele cha
maadhimisho ya siku ya wazeeduniani yaliyofanyika kitaifa mkoani
Mbeya. 1.10.2016
Na Erasto Ching’oro na rehema Kasimoto, Rujewa- Mbarali, Mbeya
Lengo ni kuondoa kero kwa wazee katika kupata Huduma za Afya
Waziri
wa Afya kupeleka Bungeni Mswada wa Sheria ya Taifa ya Wazee kabla ya
mwezi June 2017 ili pia kuweka wajibu wa kisheria kwa watoto na familia
kuwatunza wazee wao.
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu
amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwatambua wazee wasio
na uwezo na kuwapatia vitambulisho vya matibabu bila malipo, sambamba
na vitambulisho vya Bima ya Afya ya Jamii (CHF), kabla ya tarehe 31
Desemba 2016
Agizo
hilo amelitoa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani
yaliyofanyika kitaifa Wilayani Mbarali, Mkoa wa Mbeya. Maadhimisho hayo
yaliyoongozwa na Kauli Mbiu “Zuia Unyanyasaji dhidi ya Wazee”.
Akiongea
na hadhara iliyokusanyika kwa ajili ya maadhimisho hayo, Mhe Ummy ambye
alikuwa Mgeni Rasmi, alisema Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji
wa Sera ya Taifa ya Afya ya mwaka 2007 inayotambua kuwa wazee ni kundi
maalum linalohitaji kupewa huduma za Afya, hususani katika kuboresha
huduma za matibabu kwa wazee wasio na uwezo. “Lete barua ya utambulisho
kutoka Serikali ya Kijiji na Mtaa” ni kauli wanayokumbana nayo wazee wengi
kila wanapokwenda kupata huduma za afya katika vituo vya afya na Hospitali
za umma nchini hivyo anaamini kuwepo kwa Vitambulisho hivi kutasaidia
kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wazee nchini na hivyo
kuondoa unyanyasaji kwa wazee nchini.
Kuhusu
kauli mbiu ya Maadhimisho haya Mhe. Ummy alieleza kuwa Sera ya Wazee ya
mwaka 2003 inatuelekeza kuwatumia wazee kama Hazina ya Taifa. Na kuwa
tutumie mchango wao katika kuleta maendeleo kwa kuweka mazingira mazuri
ya kuwalinda na kuwatetea wazee wetu siku zote za maisha yao ikiwa ni
pamoja na kuzuia vitendo vya unyanyasaji.”
Pamoja na
jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali katika kuwalinda na
kuwaenzi wazee nchini bado wazee wetu hasa walio vijijini wanafanyiwa
vitendo vya unyanyasaji na ukatili ambavyo sio tu vinarudisha nyuma
ustawi wao bali pia kuwanyima haki yao ya msingi ya kuishi. Na
kinachosikitisha zaidi, vitendo hivi vya unyanyasaji vinafanywa katika
jamii zetu, katika koo zetu na katika kaya zetu na watu wenye wajibu wa
kuwalinda wazee hawa wengine wakiwa ndugu zao wa karibu!”.
Mhe Ummy
aliwasihi wananchi kuacha vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wazee na
vikongwe hapa nchini kwa kuwa ni jambo linalohuzunisha sana na kutia doa
Taifa letu. Wakati tukiadhimisha Siku ya wazee Duniani, mikoa
inayoongoza kwa kuwa na vitendo vingi vya unyanyasaji na ukatili dhidi
ya wazee hapa nchini ni Tabora, Geita, Mwanza na Shinyanga. Rai
inatolewa kuchukua hatua kujeweka mazingira salama kwa wazee wetu.
Mhe Ummy
aliwahakikishia wazee kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua za kisera
na kisheria kuhakikisha wazee wanalindwa na vitendo vyote vya
unyanyasaji na ukatili ikiwemo vitendo vya mauaji ya wazee ambapo sababu
kubwa ya vitendo hivi ni imani potofu na uelewa mdogo ndani ya jamii ya
Tanzania.
‘’Uzee na
Kuzeeka Hakukwepeki! Kila mtu ni mzee mtarajiwa. Hivyo kila mmoja wetu
anao wajibu wa kuwaheshimu, kuwalinda na kuwaenzi wazee wetu’’ alieleza
Mh, Ummy.
Waziri
Ummy alitoa wito kuwa na uwajibikaji wa pamoja kwa wananchi wote katika
kutokomeza vitendo vya unyanyasaji yakiwemo mauaji ya kikatili dhidi ya
wazee ‘’Serikali imepanga kupeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Taifa ya
Wazee kabla ya mwezi June 2017 ambao siyo tu itawekwa adhabu kali kwa
wote watakaokutwa na hatia ya kufanya vitendo hivi bali pia itaweka
wajibu wa kisheria kwa watoto wa familia husika na ndugu wa karibu
kuwalea na kuwatunza wazee wao’’.
Maadhimisho
ya Siku ya Wazee Duniani hufanyika kila tarehe 1 Octoba ya kila mwaka
lengo likiwa ni kutafakari hali ya maisha ya wazee na changamoto
zinazowakabili wazee; na hivyo kuweka mipango thabiti ya kuboresha
maisha yao na kuwafanya waishi maisha ya heshima, hadhi, na kuthaminiwa
utu wao.(P.T)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269