Serikali ya Kenya imewasilisha jina la
Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Bi. Amina Mohamed kuwa mwenyekiti
ajaye wa Tume ya Umoja wa Afrika AU.
Bi. Mohamed atachuana na Agapito Mba Mokuy wa Equatorial
Guinea, Abdoulaye Bathily wa Senegal na Pelonomi Venson-Moitoi wa
Botswana ambao nao wanataka uenyekiti huo.
Akitoa taarifa kuhusu Kenya kumpendekeza Bi. Mohamed kuwania wadhifa
huo, Rais Uhuru Kenyatta amesema, "Naona Amina amekuwa na utendaji kazi
mzuri na hivyo tumempendekeza kuwa Mwenyekiti wa Tume ya AU,"
Uchaguzi wa wanachama wa Tume ya AU ulikuwa ufanyike Kigali, Rwanda,
Julai 2016 wakati wa mkutnao wa kilele wa viongozi wa Afrika lakini
baada ya duru saba za upigaji kura, hakuna yeyote kati ya wagombea
watatu aliyepata thuluthi tatu za kura zinazohitajika kushinda.
Kiti hicho kiko wazi baada ya kumalizika muda wa mwenyekiti wa sasa,
Bi. Nkosazana Dlamini-Zuma wa Afrika kusini ambaye aliteuliwa mwaka 2012
lakini hakuwania tena muhula wa pili. Uchaguzi huo unatazamiwa
kufanyika Januari 2017. Bi. Mohamed amewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa na pia naibu mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
la Mazingira UNEP mbali na kushikilia nyadhifa mbali mbali katika Wizara
ya Mambo ya Nje ya Kenya.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269