Mkurugenzi wa FBI,James Comey
Mkurugenzi
wa FBI,James Comey ameliambia bunge la Marekani kuwa baada ya kupitia
barua pepe zilizogundulika kutoka kwa Hillary Clinton, wakati alipokua
waziri wa mambo ya nje wamegundua kuwa hana hatia yoyote na
hawatamfungulia mashtaka.
Kampeni
za Clinton ziliingia doa wiki iliyopita baada ya mkurugenzi huyo wa FBI
kusema kuwa watazipitia barua pepe zake zilizopatikana katika kompyuta
ya msidizi wa zamani wa mume wake.
Kauli hiyo imeonekana kumfurahisha mkuu wa mawasiliano wa kampeni za Clinton Jennifer Palmieri
Donald Trump,mgombea urais nchini Marekani
Wakati
upande wa Bi Clinton wakifurahia hatua hiyo kwa upande wake Donald Trump
amesema Hillary Clinton analindwa na mfumo wa wizi wa kura, amesema Bi
Clinton angetakiwa kuchunguzwa kwa muda mrefu.
Na hivi
sasa tunaunana moja kwa moja na Zuhura ebu tuambie baada ya FBI kusema
hawatamshtaki Hilary Clinton, hali ikoje kwa sasa ikiwa ndio imebaki
takribani siku moja uchaguzi ufanyike.BBC
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269