Mkuu
wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa
kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza,
Sekour Toure, hii leo.
Na BMG
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa
kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza,
Sekour Toure
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akizindua jengo la kituo cha One Stop
Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akizindua jengo la kituo cha One Stop
Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akizungumza wakati wa ufunguzi wa
kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza,
Sekour Toure
Antony
Binamungu ambaye ni mlinzi wa mtoto na ukatili wa kijinsia kutoka
shirika la PACT Tanzania, akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mwakilishi
kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Notigela Ngaponda, akizungumza kwenye uzinduzi wa Kituo cha Pact
Tanzania
Viongozi mbalimbali
Mwakilishi
kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Notigela Ngaponda, akizungumza na wanahabari ambapo amesema kituo hicho
kitarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia.
Baadhi ya watumishi wa hospitali ya Sekour Toure
Na George Binagi-GB Pazzo
Mkuu wa mkoa
wa Mwanza John Mongella amewataka maafisa ustawi wa jamii kwa kushirikiana na
askari polisi kitengo cha dawati la jinsia, kufikisha elimu ya kupambana na
ukatili wa kijinsia kwa wananchi ili kusaidia mapambano dhidi ya vitendo hivyo.
Mongella
ametoa agizo hilo wakati akifungua kituo cha huduma Shirikishi dhidi ya Ukatili
wa kijinsia na watoto cha One Stop Centre kilichojengwa na taasisi ya Pact
Tanzania kwa ufadhiri wa watu wa Marekani, katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Mwanza Sekour Toure.
Amesema
hatua za kukabiliana na ukatili wa kijinsia zinapaswa kuchukuliwa
mapema badala ya kusubiri utokee katika jamii ambapo amesema watakaokuwa
wakipatikana na hatia za kujihusisha na ukatili wa aina hiyo
watachukuliwa hatua za kisheria mara moja.
Mganga Mkuu
wa Hospitali ya Sekour Toure, Dkt.Leonard Subi, amesema kituo hicho
kitajumuisha watumishi mbalimbali ikiwemo polisi, maafisa ustawi wa jamii
pamoja na wataalamu wa afya kwa ajili ya kuwahudumia wahanga wa vitendo vya
ukatili wa kinjinsia ambavyo bado vimeshamiri mkoani Mwanza.
Amebainisha
kwamba kwa kipindi cha mwezi julai hadi septemba, wananchi 238 mkoani
Mwanza wamepatiwa huduma za ukatili wa kijinsia katika hospitali na
vituo mbalimbali vya afya na kati ya hao 77 ni ukatili wa watoto. Kituo
hicho tayari kimehudumia watu wazima 30 waliolengwa na ukatili wa
kijinsia huku watoto wakiwa ni 67.
Naye
Antony Binamungu ambaye ni mlinzi wa mtoto na ukatili wa kijinsia
kutoka shirika la PACT Tanzania, amesema ujenzi wa kituo hicho
umegharimu shilingi milioni 80 ikiwa ni pamoja na gharama za vifaa na
mafunzo ambapo kinakuwa kituo cha nane nchini miongoni mwa vituo vya One
Stop Centre.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269