Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia
nguo zinazotengenezwa na Kiwanda cha A to Z,kulia ni Mkurugenzi wa kiwanda
hicho Bw.Kalpesh Shah.
Makamu
wa Rais amefanya ziara kwenye kiwanda hicho ikiwa sehemu yakutambua
mchango wa wawekezaji wa ndani na changamoto wanazokutana nazo ili
kupata majibu ya kurahisisha kufanikisha Tanzania mpya ya Viwanda.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia
namna nguo zinazotengenezwa na Kiwanda cha A to Z kilichopo Kisongo
mkoani Arusha,kulia ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw.Kalpesh Shah.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata
maelezo ya namna kiwanda cha A to Z kinavyofanya utafiti wa kupambana na wadudu
wanaoharibu Mahindi kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo cha utafiti cha Africa
Technical Research Centre Dkt.Johson Ouma Odera.
.......................................................................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuviimarisha vyuo vya
ufundi stadi nchini –VETA- ili viweze kutoa wahitimu bora ambao watakidhi
katika soko la ajira hasa kwenye viwanda vilivyopo na vitajengwa nchini.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa
kauli hiyo leo wakati anazungumza na uongozi wa kiwanda cha A to Z kilichopo
mkoani Arusha katika ziara yake ambayo imeingia siku ya Pili ya kutembelea
viwanda mbalimbali mkoani humo ili kujua changamoto zinazokabili viwanda hivyo
na serikali kuzitafutia ufumbuzi.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema
serikali imetenga fedha za kutosha zitakazotumika kuviimarisha vyuo vya Veta
ili viweze kutoa mafunzo bora yatakayosidia vijana kufanya kazi zao kwa ufanisi
wa hali ya juu pindi watakapoajiriwa au kujiajiri wenyewe.
Kuhusu maslahi kwa wafanyakazi wa Kiwanda cha
A to Z,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameutaka uongozi wa kiwanda
hicho kulinda na kutetea haki za wafanyakazi kwa kutoa maslahi mazuri ambayo
yatawezesha wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii.
Makamu wa Rais pia amesisitiza usawa katika
ulipaji wa mishahara kwa wafanyakazi wa ndani na wa nje ya nchi walioajiriwa kwenye
kiwanda hicho ili kuondoa tofauti za mishahara hali ambayo ijenga motisha kwa
wafanyakazi.
Kiwanda cha A to Z kilichopo eneo la Kisongo
mkoani Arusha ambacho kinatengeneza vyandarua, nguo na mifuko mbalimbali
ikiwemo ya saruji kimeajiri zaidi ya wafanyakazi 7500 ambapo asilimia 80 ya
wafanyakazi wote ni wanawake.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
amewahimiza wawekezaji kote nchi walipe kodi za serikali mapema kodi ambazo
zitatumika kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Amewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania
itaendelea kujenga na kuimarisha mazingira bora kwa wawekezaji ili kuhakikisha
wawekezaji wanafanyakazi zao vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa na ya
wawekezaji.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269