MAREKANI:
Mgombea Urais wa Chama cha Republican, Donald Trump ameshinda kiti
hicho. Trumpa ambaye mpaka sasa ana kura 288 huku Hillary Clinton akiwa
na kura 218 za wajumbe kati ya kura zote 538.
Kwa
mujibu wa Katiba ya Marekani, Mshindi wa urais alitakiwa kushinda
angalau kura 270 kati ya hizo 538 lakini Bw. Trump amevuka na kufikisha
kura 279 mpaka sasa.
Clinton akubali kushindwa
CNN na NBC wameripoti kwamba mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton amempigia simu Donald Trump na kukubali kushindwa.
Shangwe kambi ya Trump
Shangwe, nderemo na vifijo zimetanda miongoni mwa wafuasi wa Donald Trump.
Trump: Asanteni sana
Trump
amepanda jukwaani Manhattan, New York. Amewashukuru wafuasi wake na
kusema amepigiwa simu na Hillary Clinton “kuwapongeza”.
Akizungumza
na wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi, Trump amewataka raia wote
wa Marekani, waliomchagua na ambao hawakumchagua kuungana na kuanza
kuijenga nchi yao kwani muda wa kampeni na siasa za kugawanyika
umekwisha.(P.T)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269