Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Monica
Mnanka (kushoto), akizungumza na waandishi wa habariwakati akimkaribisha
msajili wa vyama kuzungumza na wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi.
Kulia ni Msaji Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza na Msajili wa
Vyama, Jaji Francis Mutungi.
Msajili
wa VVyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi (kushoto), akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa
taarifa ya kufutwa kwa usajili wa kudumu wa vyama vitatu vya siasa
ambavyo ni Chama cha Haki na Ustawi (Chausta), chama cha The African
Progressive Party of Tanzania (APPT Maendeleo) na Chama cha Jahazi
Asilia. Kulia ni Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
MSAJILI
wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi kwa mamlaka aliyonayo
chini ya kifungu cha 19 cha Sheria ya vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka
1992, amevifutia usajili wa kudumu vyama vitatu vya siasa kuanzia leo
hii.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake leo asubuhi Jaji Mutungi alivitaja Vyama alivyovifuta kuwa ni Chama
cha Haki na Ustawi (Chausta), kilichopata usajili wake Novemba 15, 2001
kilichokuwa kikiongozwa na James Mapalala kama Mwenyekiti wa Taifa na
Mwaka Lameck Mgimwa kama Katibu Mkuu.
Chama
kingine alichokifutia usajili wa kudumu ni Chama cha The African
Progressive Party of Tanzania (APPT Maendeleo) kilichopata usajili
Machi 4, 2003 kilichokuwa kikiongozwa na Peter Kuga Mziray kama Rais
Mtendaji Taifa na Nziamwe Samwel kama Katibu Mkuu.
Jaji
Mutungi alikita chama kingine alichokifuta kuwa ni Chama cha Jahazi
Asilia kilichokuwa kikiongozwa Kasimu Bakari Ally kama Mwenyekiti wa
Taifa na Mtumweni Jabir Seif kama Katibu Mkuu ambacho kilipata usajili
wa kudumu Novemba 17, 2004.
Mutungi
alisema vyama hivyo vimepoteza sifa za usajili wa kudumu kwa kukiuka
masharti ya Sheria ya Vyama vya Siasa, ambapo kila chama klipewa taarifa
ya nia ya Msajili wa Vyama vya siasa kufuta usajili wake wa kudumu na
kutakiwa kueleza kwanini kisifutwe ambapo vilishindwa kutoa sababu za
kuridhisha kuwa havikukiuka sheria na bado vinavyo sifa za usajili wa
kudumu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269