Waziri
wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe yuko mkoani
Mbeya kuangalia utendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara yake na
kuzungumza na watendaji ndani ya taasisi hizo.
Katiba
Ziara hiyo Dkt Mwakyembe alianza kwa kutembelea kituo cha usajili watoto
chini ya umri wa miaka mitano na kupatiwa cheti cha kuzaliwa kilichopo
Katiba jiji la Mbeya.
Akizungumza
katika kituo hicho Dkt Mwakyembe ameutaka uongozi wa mkoa wa Mbeya
kuhakikisha zoezi hilo la usajili watoto Ili wapatiwe vyeti vya kuzaliwa
linakuwa na mafanikio kama ilivyo katika Mikoa ya Iringa na Njombe
ambayo imeandikisha watoto wao kwa asilimia 98 ndani ya miezi miwili
tangu mpango huo uzinduliwe katika mkoa wa Iringa mwezi Septemba Mwaka
2016.
Amesema
usajili wa watoto hao na raia wengine kunaiwezesha nchi kupanga
kikamilifu mipango yake ya maendeleo kwani itaiwezesha nchi kuzingatia
mahitaji husika kwa mujibu wa takwimu zilizopo.
Akiwa
Mahakama Dkt . Mwakyembe amewapongeza Majaji na Mahakimu kwa kujitoa
Kwao na kufanikisha azma ya upunguzaji wa mlundikano wa kesi uliokuwa
ukiikabili Mahakama ndani ya kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Amesema
kiwango walichojiwekea Majaji na Mahakimu kimesaidia sana kufanikisha
suala la mlundikano wa mashauri ya wananchi yaliyopo mahakamani
yanamalizwa na mengine kwa wakati.
Dkt
Mwakyembe pia alitembelea Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali mkoani
humo na kuzungumza na wafanyakazi wa ofisi hiyo na kuwapongeza kwa kazi
kubwa ya kuitetea Serikali Mahakamani wanayoifanya na kuwaeleza kuwa
Serikali ya awamu ya Tano inathamini mchango wao mkubwa wanaoutoa na
kuokoa Mali na fedha za umma.
Waziri
Mwakyembe pia ametembelea gereza la Ruanda la mkoani Mbeya na kuzungumza
na maafisa wa Jeshi la Magereza na wafungwa na mahabusu walioko ndani
ya gereza hilo.(P.T)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269