Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akizungumza na baadhi ya
viongozi wa Serikali wakati wa kumuaga aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero, ambapo
alimshukuru kwa jitihada zake katika kusaidia upatokanaji wa mikopo kwa
ajili ya kutekeleza miradi ya Barabara, nishati, kilimo na elimu, Makao
Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) na aliyekuwa
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia
Kandiero wakifurahia uhusiano mzuri uliopo kati ya Benki ya AfDB na
Tanzania ambapo mpaka sasa miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo inafikia
thamani ya Dola za Marekani Bilioni 2, wakati wa kuagwa kwa Dkt.
Kandiero, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
Aliyekuwa
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia
Kandiero akitoa maneno ya shukrani mbele ya Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), wakati akiagwa na Waziri
huyo, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akipeana mkono
na aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
Dkt. Tonia Kandiero (kulia), baada ya kuagwa rasmi, katika Makao Makuu
ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akimkabidhi
zawadi ya shukrani aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero (kulia) wakati akiagwa rasmi baada ya
kupewa majukumu mengine ya Ukurugenzi Mkuu wa Benki ya AfDB kusini mwa
Afrika, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es
salaam.
Baadhi ya
Wakuu wa Idara na Taasisi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa
tayari kumuaga aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero baada ya kufanya kazi nchini kwa
takribani miaka sita, Makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini
Dar es salaam.
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269