Sakata na
kifo cha Faru John (38), limechukua sura mpya baada ya wahifadhi wa
eneo la Sasakwa Singita Grumet kueleza kuwa hakuna kaburi lake kwa kuwa
hakuzikwa.
Wamesema hayo siku moja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutangaza kuunda timu mpya kuchunguza mazingira ya kifo cha faru huyo huku akihoji mambo manne yaliyozua utata.
Mambo aliyohoji wakati akifanya majumuisho ya ziara yake mkoani Arusha ni juzi, Faru John aliumwa lini, aliumwa nini, daktari gani aliyemtibu na zilipo taarifa za matibabu yake.
Wamesema hayo siku moja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutangaza kuunda timu mpya kuchunguza mazingira ya kifo cha faru huyo huku akihoji mambo manne yaliyozua utata.
Mambo aliyohoji wakati akifanya majumuisho ya ziara yake mkoani Arusha ni juzi, Faru John aliumwa lini, aliumwa nini, daktari gani aliyemtibu na zilipo taarifa za matibabu yake.
Pia
aliagiza mwili wa faru huyo kufukuliwa na kutazama kama vinasaba vyake
vinaendana na watoto wake 26 ambao bado wapo katika Creta ya Ngorongoro.
Akizungumza na mwandishi wetu jana, mmoja wawahifadhi wa Sasakwa Grumet aliyeomba kutotajwa jina ili kutoathiri uchunguzi wa tukio hilo, alisema kitaalamu wanyama ambao wanakufa bila kuwa na magonjwa ya mlipuko katika maeneo ya hifadhi hawazikwi.
Akizungumza na mwandishi wetu jana, mmoja wawahifadhi wa Sasakwa Grumet aliyeomba kutotajwa jina ili kutoathiri uchunguzi wa tukio hilo, alisema kitaalamu wanyama ambao wanakufa bila kuwa na magonjwa ya mlipuko katika maeneo ya hifadhi hawazikwi.
“Faru
John baada ya kufa aliondolewa pembe zake na kutupwa ili kiwe chakula
cha wanyama wengine wanaotegemea mizoga, lakini kuna mifupa yake,”
alisema.
Alisema
faru huyo aliombwa na Grumet kwenda kupanda faru waliopo katika eneo
hilo, hasa baada ya dume aliyekuwapo huko kuuliwa na tembo.
“Baada ya kuonekana kuna haja ya kutafuta dume, ndipo tuliomba kupata faru dume na tukaletewa na baadaye alikufa,” alisema.
Eneo hilo
la Sasakwa Singita Grumet ni mali ya mfanyabiashara mkubwa raia ya
Marekani, bilionea Tudor Jones ambaye amewekeza katika maeneo kadhaa ya
uhifadhi.
Akifafanua
hatua zinazochukuliwa baada ya mnyama kufa katika hifadhi, mhifadhi
Peter Isango alisema kwa kawaida huzikwa au kuchomwa moto pale tu
wanapobainika kuwa na magonjwa kama kimeta.
Kauli
hiyo iliungwa mkono na mkurugenzi mkazi wa shirika la uhifadhi la
kimataifa la Frankfurt Zoological Society, Gerald Bigurube ambaye
alisema kwa kawaida wanyama wanaokufa hifadhini huwa hawazikwi.
Bigurube
ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa
(Tanapa) alisema kwenye kanuni za uhifadhi kitu chochote, kinachokufa
ndani ya hifadhi huachwa kwa ajili ya kulinda ikolojia na bionuwai.
“Mnyama ambaye anakufa kwa kifo cha kawaida mzoga wake unapaswa kuachwa kuoza na kutumiwa na wanyama wengine,” alisema.
Alisema
hata wanyama wa kawaida kama swala na wengine wanapoumwa huwa hawatibiwi
tofauti na wanyama kama tembo, faru na wengine wakubwa ambao hutibiwa.
Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu Faru John, Bigurube alisema taasisi yake haikuwahi kushiriki katika suala hilo.
Wapata dhamana
Katika
hatua nyingine, Polisi imewaachia kwa dhamana maofisa watano wa Mamlaka
ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Tanapa waliokuwa wanashikiliwa kwa
tuhuma za kumhamisha Faru John kutoka Creta ya Ngorongoro na kumpeleka
Sasakwa Grumet.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema jana kuwa licha ya dhamana hiyo, uchunguzi unaendelea.
Watuhumiwa
hao ni Israel Naman ambaye alikuwa kaimu mkuu wa idara ya hifadhi
wakati faru huyo akiondolewa, Cuthbert Lemanya aliyekuwa mkuu kanda ya
Creta, Dk Athanas Nyaki ambaye ni daktari wa mifugo wa mamlaka hiyo.
Wengine ni aliyekuwa kaimu mkuu idara ya maendeleo ya jamii, Kuya Sayaleli na kaimu mkuu idara ya ikolojia, Patrice Mattey.
Kabla ya
kukamatwa, maofisa hawa walikiri kushiriki kumhamisha Faru John kutoka
Creta ya Ngorongoro hadi Sasakwa kwa maelezo kuwa ilikuwa ni kuendeleza
uhifadhi wa faru na pia kutokana na ukorofi wa Faru John kuhodhi majike
yote ndani ya Creta kuua madume wengine waliozaliwa.
Akiwa
katika ziara ya kikazi mkoani Arusha, Waziri Mkuu alitoa taarifa za kifo
cha faru John huku akiwatuhumu baadhi ya watendaji wa NCAA kuhusika na
njama za kumuuza kwa Sh200 milioni ambazo alisema walishapokea malipo ya
awali ya Sh100 milioni.
Baada ya
maelezo hayo, Waziri Mkuu alitaka kupewa taarifa kamili za tukio hilo,
pamoja na pembe za faru huyo, ambazo alikabidhiwa Desemba 8 na Waziri wa
Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na kaimu mkurugenzi wa
msaidizi kitengo cha kupambana na ujangili, Robert Mande ambaye
alimweleza kuwa taratibu zilifuatwa katika kumhamisha.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269