Kitengo Cha Ubora wa
Samaki na Udhibiti wa Rasilimali za Uvuvi Kanda ya
Kigoma imewataka Wavuvi waache kuvua Dagaa aina ya Kauzu na Ugala waliopo katika
Ziwa Tanganyika lililopo Mkoa wa Kigoma, na wazingatie sheria ya uvuvi ya mwaka 2009 na kanuni za mwaka
2005,ili wafanye shughuli zao kwakulinda na kuhifadhi mazalia ya samaki na
dagaa waliopo katika ziwa hilo.
Akizungumza na
Jamboleo jana katika Ofisi za kanda hiyo
iliyopo Mwalo na Kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji Ofisa Mfawidhi
kitengo hicho Rodlick Mahimbali alisema
kutokana na wadau wa mazao ya ziwa Tanganyika(samaki,dagaa) kukiuka sheria za
uvuvi bora,kitengo hicho kimefanikiwa kukusanya kiasi cha fedha sh.Milioni 21.5 katika kipindi cha
miezi mitatu tu,kwa maana ya Octoba hadi Desemba 2016.
“wamiliki wa mitumbwi ya kuvulia samaki na dagaa wanajua
wajibu wao,ni pamoja na kununua nyavu rafiki wa kulinda mazalia ya samaki na
dagaa,ambapo zana aina ya nyavu zote
ziwe zaidi ya Nchi tatu na si chini ya
Nchi mbili,lakini wao wanapenda kutumia makokoro,neti za mbu ambazo kiujumla
wanavua watoto wa samaki na wanaharibu mazalia” alisema Ofisa Mahimbali.
Alifafanua kuwa,ili kulinda na kuhifadhi vizazi vya dagaa na
samaki Wavuvi hawana budi watumie zana za uvuvui zenye kiwango cha ubora wa
nyavu zenye zaidi ya nchi 3 sanjari na
kuvua kwenye kina kirefu cha maji,ambako kuna samaki wakubwa wenye tija
ya kuimasrisha afya za walaji na si bora kuvua ambayo inawaghalimu pindi
wanaposhikwa na serikali kwa kupewa adhabu ya faini na kuharibiwa zana haramu.
Mahimbali aliongeza kwa kusema serikali ina lengo la kulinda
mazao hayo ili yawe endelevu kwa leo na kiazazi kijacho na uvuvvi haramu ni
kikwazo kwa taifa kujiendesha kitaalamu
katika kukuza uchumi wa mtu binafsi na taifa kwa ujumla na kuwashauri
washirikiane kuwaibua wamiliki na wavuvi wanaovunja sheria ya uvuvi ya mwaka
2009,ili kudhibiti uvuvi wa zana haramu.
Alipohojiwa Mwenyekiti
wa Chama Cha Wavuvi mkoani humu Sendwe
Ibrahimu alisema uhalisia wa mambo hakuna mmiliki na mvuvi asiyejua wajibu wake
katika sekta ya mazao ya ziwani,lakini kutokana na changamoto ya zana bora za
uvuvi ndio chanzo cha uvuvi haramu,mitumbwi haina uwezo wa kufika katika kina
stahiki sana cha maji hali inayowalazimu wavue karibu na mazalia ya samaki.
Aliwashauri wadau wa sekta hiyo watumie vikundi mtambukwa
kuwakopesha zana za kisasa za uvuvi,ili wavue samaki katika kina kirefu cha
maji(gazini) kwa lengo la kuvua samaki na dagaa wakubwa ambao bado hawajavuliwa
tangu kuumbwa kwa dunia kwa kuwa zana wazitumizo ni za kale ambazo hushawishi
baadhi kutumia zana haramu hasa neti za mbu,makokoro na sumaku ni nyavu za nchi ya Burundi,ambayo haichagui samaki wala dagaa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269