Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kushoto)
akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa jengo jipya la Ubalozi wa India
lililopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam
Balozi wa
India hapa nchini Bw. Sandeep Arya (wa pili kushoto) akimuonesha Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan picha mbali
mbali zenye kuonyesha historia ya urafiki baina ya Tanzania na India
wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la ubalozi wa India jijini Dar es
Salaam.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa ufunguzi wa Jengo jipya la Ubalozi wa India hapa
nchini.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa ufunguzi wa Jengo jipya la Ubalozi wa India
lililopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam.
Balozi wa India hapa nchini Bw. Sandeep Arya akihutubia wakati wa uzinduzi wa Jengo jipya la Ubalozi wa India hapa nchini.
Vikundi vya Utamaduni wa Kihindi vikionyesha uwezo wa kuzicheza ngoma za asili.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassana
ameishukuru Serikali ya India kwa ufadhili wake wa miradi ya maji katika
miji 17 nchi ambayo inalenga kupunguza tatizo la maji kwa wananchi
wengi nchini.
Makamu wa
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam
katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 68 ya Siku ya Kitaifa ya Jamhuri ya
India sherehe ambazo zimeambatana na Uzinduzi rasmi wa majengo ya ofisi
mpya ya Ubalozi wa India hapa nchini.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema ufadhili wa miradi ya Maji pamoja
na miradi mingine unaofanywa na Serikali ya India kwa Tanzania Bara na
Zanzibar unadhihirisha wazi mahusiano mazuri yaliyopo yaliyoasisiwa na
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mahatma Gandhi wa India.
Makamu wa
Rais amesisitiza kuwa India ni moja ya washirika muhimu katika juhudi
za kuwaletea wananchi maendeleo na Serikali itaendelea kufanya kazi kwa
karibu katika maeneo mengi ikiwemo ya kikanda na kimataifa kwa ajili ya
manufaa ya wananchi wa pande Mbili yaani Tanzania na India.
Amesema
kwa miaka mingi sasa mahusiano ya kindugu yamekuwa yaakiimarika katika
sekta mbalimbali ikiwemo kisiasa,kidiplomasia,kibiashara, masuala
ulinzi, utamaduni na mwingiliano wa watu na watu.
Makamu wa
Rais pia ameishukuru Serikali ya India kwa msaada wake wa shilingi
milioni 500 alioutoa kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera ambao walikubwa na
tetemeko la ardhi mwaka jana.
Ameeleza
kuwa Mahusiano kati ya India na Tanzania yamekuwa na manufaa makubwa
ambapo idadi kubwa ya watanzania wanaenda kupata mafunzo mbalimbali
nchini India hasa Madaktari na wamekuwa msaada mkubwa katika kuokoa
maisha ya Watanzania.
Katika
hafla hiyo, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye hotuba yake alitoa
salamu za rambirambi kwa Serikali ya India kufuatia ajali ya treni
iliyotokea katika Jimbo la Andhra Pradesh na kusababisha vifo vya watu
30 na kujeruhi wengine.
“Kwa
niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania napenda
kutoka salamu za Pole kwa familia za wafiwa na majeruhi katika kipindi
hiki kigumu kwa kumwomba Mwenyezi Mungu azipumzishe roho za marehemu
mahali pema peponi na tunawaombea majeruhi wapone haraka. ’’
Kwa
upande wake, Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya amemhakikishia
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Serikali ya India itaendelea
kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kwa ajili ya manufaa
ya wananchi wa pande zote Mbili.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269