Mkurugenzi
wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agenes
Mtawa akimkabidhi vitanda Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Kibiti, Ayub
Ngereza kutokana na hospitali ya halmashauri hiyo kuwa na upungufu wa vitanda
vinavyotumiwa na kinamama wakati wa kujifungua. Mhandisi Ngereza
amepokea msaada wa vitanda hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Kibiti.
NA JOHN STEPHEN, MNH
KATIKA
kuendelea kuboresha mazingira ya utoaji huduma ya afya ya uzazi kwa akina mama,
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imetoa msaada wa
vitanda viwili vya kujifungulia kwa Hospitali ya Wilaya ya Kibiti
mkoani Pwani.
Akikabidhi
vitanda hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
, Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Agnes Mtawa, (pichani anayezungumza na waandishi), amesema lengo
ni kuboresha huduma za afya na kumuwezesha mama kujifungua katika mazingira
salama.
"Wenzetu
wanahuitaji mkubwa wa vitanda vya kujifungulia hivyo tumeona tuwasaidie, natoa
wito kwa Watanzania watambue kwamba hospitali hizi ni za kwetu na zinawahudumia
Watanzania hivyo wale wenye nafasi ya kusaidia ni vema wakafanya hivyo ili
kuendelea kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto" amesema Sister Mtawa.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi huyo wa Huduma za Uuguzi na Ukunga tatizo la ukosefu wa
vitanda husababisha Mkunga kupata shida wakati mama anapojifungua.
Naye Mhandisi
Ujenzi wa Halmashauri ya Kibiti, Ayub Ngereza akipokea msaada huo
kwa niaba ya Mkurugenzi wa wilaya ya Kibiti, ameushukuru uongozi wa Hospitali
ya Taifa Muhimbili kwa msaada huo kwani utasaidia kuboresha huduma
za afya.
Hivi
karibuni Hospitali ya Taifa Muhimbili ilikabidhi msaada
wa vitanda vitano vya kujifungulia kwa Hospitali ya wilaya
ya Mafya ambapo kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa
Hospitali hiyo Abdalah Bhai walihitaji vitanda vitano ambao ulikidhi mahitaji.
Mhandisi
Ngereza akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kukabidhiwa vitanda
hivyo na uongozi wa hospitali hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa
Halmashauri hiyo wakipakia vitanda hivyo kwenye gari leo
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269