Naibu
Waziri wa Wizar ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisindikizwa
na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelote Stephen mara baada ya kumaliza kupokea taarifa
ya mkoa na taarifa ya vyombo vya usalama mkoa huo wakati wa ziara ya kikazi mkoani
hapo.
(PICHA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelote Stephen akitoa
taarifa ya mkoa na taarifa ya vyombo vya usalama mkoa huo kwa Naibu Waziri wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni(kulia), wakati wa ziara ya Naibu Waziri kutembelea idara zilizopo
chini ya wizara yake.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni, akizungumza wakati alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza mkoa
wa Rukwa kwa ziara ya kikazi, Kulia ni wakuu wa jeshi hilo mkoani hapo wakimsikiliza.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi Selemani Kameya
akisoma taarifa ya utendaji kazi ya Mkoa huo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa ziara ya kikazi ya
Naibu Waziri huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, ACP George
Kyando akizungumzia Mradi wa Ujenzi wa ofisi wakati Naibu Waziri wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipotembelea jengo hilo kuona
maendeleo ya mradi huo na kuwataka kutumia rasilimali watu ya wafungwa waliopo
mkoani hapo ili kuweza kukamilisha ujenzi huo wakati wa ziara ya kikazi
aliyoifanya mkoani hapo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea risala kutoka kwa askari wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji mkoani Rukwa mara baada ya kuisoma kwa niaba ya wenzake ikiwa na
maombi mbalimbali yaliyoelekezwa kwa wizara.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Simiyu, Paul Mzindakaya baada ya kumaliza kupokea taarifa ya hali ya usalama
mkoani Rukwa wakati Naibu Waziri alipokuwa mkoani humo kwa ziara ya kikazi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269