Naibu
waziri wa Nishati na madini Dr,Merdadi Kalemani akiwasilia katika
mgodiwa wa RZ ambako kumetokea tukio la watu 14 kufukiwa na udongo
wakati wakiendelea na kazi za uchimbaji.
Mbunge wa Jimbo la Busanda ,Lorencia Bukwimba akielekea kwenye eneo la shimo ambapo watu wamefunikwa.
Mbunge wa
Jimbo la Busanda ,Lorencia Bukwimba akiwapa pole ndugu na jamaa ambao
walikuja kujua kile ambacho kitaendelea kwa undugu zao.
Wananchi wakiwa nje ya Ngome ya mgodi wakifatilia kile ambacho kinaendelea
Sehemu ambayo inatumiwa kutolea udongo.
Ndugu wakiwa katika masikitiko makubwa wakijiuliza ni lini ndugu zao watatoka shimoni.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Ezekiel Kyunga akiwa katika eneo la tukio akifatilia kile kinachoendelea
Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi akipandisha juu baada ya kutoka shimoni
Naibu waziri wa nishati na madini,Dr Medadi Kalemani akioneshwa baadhi ya maeneo yaliyopata dosari kwenye mgodi huo
NA MADUKA ONLINE
NAIBU
waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani ametembelea Mgodi wa RZ
uliofukia Watanzania 13 na raia mmoja wa Nchini China anayetambulika kwa
jina la Meng Juping na kusema kuwa serikali itaendelea kuweka nguvu ili
kusaidia uokoaji.
Katika
ziara yake hiyo ya dharura Naibu Waziri huyo ametoa pole kwa niaba ya
serikali kwa uongozi wa Mkoa, Wananchi pamoja na....
Mgodi huo kukumbwa na tukio hilo.
Mgodi huo kukumbwa na tukio hilo.
Mara
baada ya kupokea taarifa ya maafa hayo, iliyosomwa na kamishina msaidizi
wa madini kanda ya ziwa victoria, Dk. Kalemani aliutaka uongozi wa Mkoa
pamoja kamati ya uokoaji kujikita zaidi kwenye shughuli ya uokojai na
waachane na mambo mengine ambayo yanaweza yakasababisha zoezi hilo liwe
gumu.
‘’Ndugu
zangu mimi kwa niaba ya serikali kuu napenda nitoe pole kwa hiki
kilichowakumba Mkoa pamoja na Mgodi lakini napenda kuwaambia kuwa Kamati
ya ulinzi na Usalama pamoja natimu ya uokoaji mhakikishe mnasimamia
vyema zoezi hili ili tuwaokoe ndugu zetu ambao wamo humo ndani ya
shimo,’’alisema Naibu waziri Kaleman.
‘’Kingine
niagize hapa hakikisheni mnatoboa shimo kwa kutumia drilling ili tupate
mwanya wa kuwapatia chakula ndugu zetu ambao wamefukiwa na udongo
wakati juhudi za kufukua zikiendelea ,’’aliongeza.
Akizungumza
na Maduka online mapema asubuhi ya leo kamishina msaidizi wa madini
kanda ya ziwa victoria Yahaya Samamba alisema kuwa kamati ya uokozi kwa
kushirikiana kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Geita, ilibadilisha
mfumo wa uokoaji kwa kutumia wachimbaji wadogowadogo baada ya mashine za
kisasa kufikia usawa mita 20 ambazo haziwezi kuhimili uzito.
‘’Mitambo
hii imekomea mita 20 tumeona tutumie wachimbaji wadogo ili twende
sambaba na uokoaji uliosalama..kwahiyo usiku wa jana (juzi) saa 5:00
kamili usiku tulisitisha kutumia mashie yaani Magreda kutokana na usawa
tuliofikia kuwa laini,’’alisema Samamba.
Kwa
upande wake Mhandisi kutoka kampuni ya uchimbaji ya Busolwa Mine Eng.
Nayompa wakati akitoa mtazamo wake namna zoezi hilo linavyokuwa gumu
alisema ramani zinazotolewa na wachina ni za kubahatisha na hawana
uhakika nazo ndizo sababu zimechelewesha uokoaji na zoezi kuonekana
halikamiliki kwa wepesi.
“Mimi
ninachokiona hapa wachina hawa ndugu zetu wachina wameshindwa kutupatia
ramani ya uhakika ndiyo maana tunabahatisha bahatisha tu..mwandishi hata
wewe jana ulikuwa shuhuda namna gari la kutoboa lilivyoshindwa kulenga
kwenye shimo walipo ndugu zetu,’’alisema Eng. Nayompa.
Kwa
upande wake Mbunge wa jimbo la Busandwa ambako tukio hilo limetokea
Lolensia Bukwimba alisema haipaswi watu kunyosheana kidole kwa sasa
wakati nguvu na jtighada zikiendelea kufanywa.
Hata
hivyo Rais wa shirikisho wa vyama vya wachimbaji wa madini ,John Wambura
Bina,amepongeza juhudi ambazo zinafanyika kwa makapuni ya madini
kujitolea pamoja na serikali na wanaamini kuwa juhudi za uokoaji
zinazoendelea zinaweza kuzaa matunda.
Viongozi
mbalimbali wa serikali na chama jana walitembelea eneo la Mawemeru
kuliko mgodi wa RZ ambao unamilikiwa na wawekezaji wa Kichina huku
leseni ya madini ikiwa ni ya Mtanzania Ahamed Mbaraka.
Matumaini
kwa siku ya leo yanaonekana kwani hadi kufikia majira ya saa moja
kamili watu ambao wapo chini waligonga bomba kwa kuashiria kuwa wapo
karibu na sehemu ya kutokea.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269