Breaking News

Your Ad Spot

Jan 29, 2017

MAHAFALI YA 32 CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT) DAR ES SALAAM

raw1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa  akizungumza na uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) katika mahafali ya 32 ya Chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho na pembeni yake ni Mkuu wa Chuo hicho Prof. Zacharia Mganilwa
raw2
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof. Blasius Nyichomba (kulia), akizungumza na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika mahafali ya 32 ya Chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
raw3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihutubia kongamano la mahafali ya 32 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
raw4
Baadhi ya wahitimu wa fani za Shahada ya Uzamili, Stashahada ya Uzamili, Shahada na Diploma katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alipokuwa akihutubia kongamano la mahafali ya 32 ya Chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
raw5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwatunuku wahitimu wa fani za Shahada ya Uzamili, Stashahada ya Uzamili, Shahada na Diploma katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages