Ofisa
Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Freddy Maro, akizungumza wakati akimkaribisha
Msemaji wa Serikali kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo,
Mindi Kasiga.
Msemaji wa Serikali kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mindi Kasiga, akifurahia jambo pamoja na Ofisa
Habari wa wizara hiyo, Freddy Maro, wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo
kwa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)
jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Baadhi ya Maofisa wa SSRA na TRA, wakiwa katika hafla ya kikabidhi tuzo hizo za Umoja wa Afrika (AU) kwa taasisi hizo.
Msemaji
wa Serikali kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo, Mindi
Kasiga, akizungumza wakati wa kukabidhi tuzo za Umoja wa Afrika (AU)
katika kipengele cha Ubunifu wa mradi wa kazidata ya Taifa ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii na ushindi wa Jumla kwa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) jijini hivi karibuni.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhi tuzo hizo.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde (katikati), akiwa pamoja na Meneja
Huduma za Mlipa Kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard
Kayombo (kushoto) na Kiongozi wa Kundi la wabunifu wa Mradi wa Mifumo wa
SSRA, David Nghambi.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Taasisi yake ilivyofanikiwa kupata tuzo ya Ubunifu wa mradi wa kazidata ya Taifa ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii, iliyotolewa na Umoja wa Nchi za Afrika (AU).
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Mifuko wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Bi. Sarah Kibonde, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa tuzo hizo.
Meneja
Huduma za Mlipa Kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard
Kayombo akielezea namna Mamlaka ya Mapato ilivyofanikiwa kupata tuzo
katika kipengele cha Ubunifu wa mradi TANCIS, ambao umeunganisha mifumo
midogomidogo ya Forodha na kupelekea kurahisisha utoaji wa huduma na kuongeza ukusanyaji wa mapato, tuzo iliyotolewa na Umoja wa Nchi za Afrika (AU).
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde (kulia) akiwa na Meneja Huduma za Mlipa Kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo.
Msemaji
wa Serikali kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo, Mindi
Kasiga, akifafanua mambo mbalimbali wakati wa kukabidhi tuzo hizo. Kulia
ni Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde na katikati ni Meneja Huduma za Mlipa Kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde
akikabidhiwa cheti cha tuzo ya Ubunifu Bora katika Sekta za Kiserikali
Barani Afrika 2016.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde (kulia)
akipokea kombe la Ushindi wa jumla kwenye ubunifu wa utoaji wa huduma
katika mambo ya ushirika 2016, Barani Afrika, iliyotolewa na AU, toka
kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mambo ya Nje
ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi.
Mindi Kasiga.
Meneja Mifumo ya Forodha toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw.
Tinkasimile Felix (kushoto) akipokea tuzo ya ubunifu wa mradi TANCIS,
ambao umeunganisha mifumo midogomidogo ya Forodha toka kwa Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maofisa wa mamlaka hiyo mara baada ya kukabidhiwa tuzo hizo.
Wawakilishi
kutoka SSRA, TRA, wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilish toka
Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa mara baada ya kukabidhiwa tuzo hizo, zilizotolewa
na Umoja wa Nchi za Afrika (AU).
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde, akiwa
amekaa na kombe la ushindi wa jumla.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde,
akilifurahia kombe hilo la ushindi wa jumla.
Maofisa wa SSRA, David Nghambi (kushoto) na Ally Masaninga, wakiwa wamelishikilia kombe hilo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269