Waziri
mkuu Kassim Majaliwa amewasili mkoani Dodoma leo asubuhi kwa ajili
kuhudhuria vikao vya bunge ambavyo vinatarajiwa kuanza kesho Jumanne.
Waziri
Mkuu ameongozana na mkewe Mary Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali
ambao wametumia usafri wa ndege ya abiria ya ATCL inayopitia Dodoma
kuelekea Kigoma.
Katika
Uwanja wa Ndege Waziri Mkuu amepokelewa na mkuu wa mkoa wa Dodoma
Jordan Rugimbana pamoja na viongozi wa serikali na chama wa mkoa wa
Dodoma.
Vikao
vya Bunge vinaanza kesho baada ya wiki mbili za shughuli za kamati za
kudumu za Bunge, na sasa tayari wabunge wamekwishawasili Dodoma kwa
ajili ya vikao hivyo vitakavyodumu kwa takribani wiki 2.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269