Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya
Iran amesema kuwa taifa la Iran litajibu vitisho vilivyotolewa na Rais
Donald Trump wa Marekani katika maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya
Kiislamu ya Iran Ijumaa ijayo.
Ayatullahil
Udhmaa Ali Khamenei ambaye alikuwa akihutubia maafisa wa kikosi cha
Jeshi la Anga la Iran waliokwenda kuonana naye amesema kuwa, matamshi na
hatua za Rais mpya wa Marekani zimewadhihirishia waziwazi walimwengu
yaliyokuwa yakisemwa na Iran katika kipindi chote cha miaka 38 iliyopita
kuhusu ufisadi wa pande zote wa utawala wa Marekani.
Akizungumzia
matamshi ya Trump ambaye amesema Iran inapaswa kuishukuru serikali ya
rais aliyeondoka madarakani wa Marekani, Barack Obama, Ayatullah
Khamenei amehoji akisema: Tutaishukuru kwa kitu gani? Kwa sababu ya
kuunda kundi la kigaidi la Daesh? Kuziteketeza nchi za Iraq na Syria au
kuunga mkono uhaini wa mwaka 2009 nchini Iran?
Amesisitiza kuwa, Obama ndiye aliyeliwekea taifa la Iran vikwazo eti
vya kulemaza ingawa hakuweza kufikia lengo lake, na hakuna adui yeyote
atakayeweza kulilemaza taifa la Iran.
Kiongozi
wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, Donald Trump anapaswa kupongezwa kwa
sababu ametusaidia kudhihirisha sura na utambulisho halisi wa Marekani.
Amesisitiza kuwa, wakati wa kampeni za uchaguzi wa Rais wa Marekani na
baada yake Trump alidhihirisha waziwazi ufisadi wa kisiasa, kiuchumi,
kimaadili na kijamii wa mfumo unaotawala Marekani.
Ametilia
mkazo udharura wa kutawakali na kumtegemea Mwenyezi Mungu SW na
kutowaamini wala kutegemea mashetani hususan Shetani Mkubwa (Marekani)
na kusema: Kutegemea mashetani ni sawa na mtu mwenye kiu anayefuata
sarabi akidhania kuwa ni maji.
Mkutano
wa leo wa maafsia na wafanyakazi wa Jeshi la Anga la Iran na Kiongozi
Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu umefanyika kwa mnasaba wa tukio la
kihistoria la tarehe 8 Februari 1979 wakati maafisa wa jeshi hilo
walipotangaza baia na utiifu wao kwa Imam Ruhullah Khomeini katika
kilele cha harakati za Mapainduzi ya Kiislamu mwaka 1979.
Ayatullah Khamenei amelitaja tukio hilo kuwa lilikuwa na uhimu wa
aina yake katika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa:
Jeshi la Anga la kipindi cha utawala wa taghuti (Shah) lilikuwa na
uhusiano wa karibu sana na utawala wa kisiasa uliokuwa tegemezi kwa
Marekani na haukudhania kuwa, kamwe ungeweza kupata kipigo kikali kutoka
kwa jeshi hilo.
Ayatullah
Khamenei amesema, ni makosa makubwa sana kuwa na imani na mashetani na
kuwa na matumaini na wale wanaopinga kuwepo kwa utawala wa Uislamu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269