WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha
Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi
hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi
wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali baada ya kuzungumza nao
Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017. Kutoka kushoto ni
Samwel Shelukindo (Ufaransa), Dkt. James Msekela (Uswisi), Mbelwa
Kairuki (China), Paul Mella (DRC), Dkt. Emmanuel Nchimbi (Brazil) George
Madafa (Italy) na Elizabeth Kiondo (Uturuki).
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa akisalimiana na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania
nje ya nchi baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam,
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa akisalimiana na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania
nje ya nchi baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU )
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wa Tanzania katika nchi
mbalimbali kuhakikisha wanatumia uwakilishi wao kutafuta wawekezaji
watakaokuja kuwekeza katika sekta ya viwanda nchini.
Amesema
mkakati wa Serikali ni kuimarisha uchumi hadi wa kati kupitia sekta ya
viwanda, hivyo jukumu la mabalozi hao ni kuhakikisha jambo hilo
linafanikiwa.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 7, 2017) alipokutana na
mabalozi wa wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi za Uturuki, Brazil,
China, Italy, Ufaransa, Jamuhuri ya Kidemkrasi ya Congo (DRC) na Uswisi.
Mabalozi
hao ni Balozi Dk. Emmanuel Nchini (Brazil), Balozi Elizabeth Kiondo
(Uturuki), Balozi George Madafa (Italy), Balozi James Msekela
(Uswisi),Balozi Samuel Shelukindo (Ufaransa), Balozi Paul Mella (DRC),
Balozi Mbelwa Kairuki (China).
“Serikali
inahitaji watu wa kuja kuwekeza katika viwanda ili kuongeza thamani ya
mazao kabla ya kuyauza nje ya nchi, hivyo jukumu lenu ni kuhakikisha
tunapata wawekezaji wenye sifa,” amesema.
Pia
Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kutumia uwakilishi wao katika nchi
hizo kwa kuhakikisha wanatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili
kuongeza idadi ya watalii wanaokuja Tanzania.
Aidha,
Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kulinda maslahi ya Taifa katika nchi
hizo ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na
mataifa hayo.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kuhakikisha
wanawatambua Watanzania wanaoishi katika mataifa hayo na kushirikiana
nao katika kutafuta wawekezaji wa kuja kuwekeza nchini.
Kwa
upande wake Balozi Mella ambaye alizungumza kwa niaba ya mabozi wenzake
alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watakwenda kutekeleza wajibu wao
ipasavyo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 7, 2017.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269