Aliyekuwa
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, amesema katika
kipindi chake cha utumishi jeshini, hatasahau kamwe tukio la milipuko ya
mabomu kwenye vikosi vya Mbagala mwaka 2009 na Gongolamboto mwaka 2011.
Aliyazungumza
hayo Ikulu, Dar es Salaam Jumatatu hii wakati akiongea na wanahabari
baada ya kuapishwa mkuu mpya wa majeshi, Jenerali Venance Mabeyo.
Jenerali mstaafu Mwamunyange alisema tangu aingie jeshini mwaka 1971,
wakati wa milipuko hiyo iliyosababisha vifo na uharibufu wa mali, ndiyo
ulikuwa mgumu zaidi kwake.
“Wakati
wa milipuko ya Mbagala na Gongolamboto nilikuwa kwenye nafasi hii (Mkuu
wa Majeshi), huu ndiyo ulikuwa wakati mgumu kwangu kwa sababu
ilisababisha vifo, mali za watu na askari , kwangu kipindi
kile kilikuwa kigumu sana,” alisema Mwamunyange.
Milipuko ya mabomu ya Mbagala, ilitokea April 2009, kwa upande wa Gongo la Mboto ilitokea Februari 2011.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269