NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA
MMILIKI
Mmoja wa duka la dawa muhimu kwa binadamu katika eneo la Kibirizi
Manispaa ya
Kigoma Ujiji ,ametiwa mbaroni katika kituo cha polisi central kwa
tuhuma za kuendesha duka la dawa kama Hospitali huku akitoa huduma
mbali mbali ikiwemo kung'oa meno wagonjwa .
Kukamatwa
kwa mmiliki huyo ni matokeo ya ukaguzi uliofanywa juzi na timu
ya idara ya afya ya Halmashauri ya Manispaa ya kigoma Ujiji ikiongozwa
na Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo, Dkt.Peter Nsanya.
Dkt.Nsanya alisema
kuwa katika ukaguzi wao wamegundua kwamba pamoja na kuendesha shughuli
mbalimbali zikiwemo za uuzaji wa madawa, kuchoma sindano, kung’oa meno na mambo
mengi ya matibabu ya afya ,
huku akijua hana taaluma ya utabibu na kibali cha kuendesha shughuli hiyo
ambapo ni kinyume cha sheria, kanuni nataratibu za wizara husika.
Akizungumzia tukio
hilo Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Hussein Ruhava amewataka wananchi hao
kutumia vituo vya afya na zahanati zilizo rasmi hasa za serikali ambazo
zinauhakika na utoaji huduma na kulinda afya zao.
Hata hivyo wananchi wa eneo hilo wameeleza kusikitishwa
kwa kitendo cha kukamatwa kwa mmiliki huyo sanjari na kufungwa kwa duka hilo ambalo
lilikuwa tegemeo lao kubwa katika upataji wa tiba wenye tija na kwa haraka.
Kwa
upande wa
Mmiliki wa duka hilo la dawa, Alex Hussein maarufu kama Ndevu alisema
taalumahiyo amepewa na mungu haoni sababu ya kukamatwa kwake kuwa
hajaharibu afya za wateja wake.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269