NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA
DIWANI wa Kata ya Kazulamimba wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma, Nuru Shakali
amesimamia zoezi la kuwafikisha Mahakamani Mwenyekiti wa kijiji cha Kazulamimba
Juma Kibuye na Ofisa Mtendaji Abduli
Mwinga kwa tuhuma za wizi wa matofali na
mchanga wa mradi wa ujenzi wa zahanati
ya kijiji hicho kinyume cha sheria, kanuni na taratibu husika.
Pia huwakata fedha kiasi cha sh.10,000
wanufaika wote wa Mradi wa Tasaf bila maelezo sahihi ya matumizi ya fedha hizo, hali inayowapa wakati mgumu
wanufaika kwa kuwa hawapewi hata risiti yenye kuonyesha uwajibikaji wa kukatwa
kwa fedha hizo kinyume cha sheria na taratibu za mfuko huo.
Hayo yamebainika juzi katika
kijiji hicho ambapo diwani akiongozana na Askari polisi wa katani humo kwa
ajili ya hatua za kisheria dhidi ya watuhumiwa hao,ambao wamehujumu mradi wa
wananchi kwa kuuza kinyemela ,tofali na
mchanga wenye thamani ya zaidi ya
milioni 2 ,bila ridhaa ya umma.
Akithibitisha hilo Nuru Shakali
alieleza kuwa,alipokea malalamiko hayo kutoka kwa wananchi na Februari,16,2,2017
alibaini uhalisia wa wizi huo baada ya mkandarasi wa zahanati hiyo kuanisha
kila hatua ya uzwaji wa tofali 9,700 sanjari na tripu 11 za mchanga ambazo zina
thamani ya zaidi ya fedha milioni 2.
Alisema amebaini uzozo mkubwa katika serikali ya
kijiji hicho kwa uda mrefu lakini amechoshwa na hulka zao,ambazo zitachangia
wananchi washindwe kuchangia nguvu zao katika miradi ijayo hali iliyomlazimu
kuchukua hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine hasa wapiga dili.
Kwa nyakati tofauti wenyeviti wa kitongoji cha kilelema A na C wa kata hiyo Jacksoni Biaga na Ramadhan Haruna
walisema tuhuma zinazowakabili viongozi
hao ni kweli kwa kuwa katika kikao kilichoketi 15, februari,2017 walikiri kwa
mandishi juu ya ubadhilifu wa mali za umma.
Waliongeza kuwa,awali viongozi
hao waliwashawishi wenyeviti wa vitongoji hivyo kuwa,wauze tofali na mchanga
kinyemela ,hali ambayo walikataa wakiwataka waitishe kikao cha umma kama
wanahitaji kufanya hivyo,lakini walitumia nyadhifa zao kuuza mali za wananchi
kinyume cha sheria,kanuni na taratibu.
Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho Gervas
Kengwa na Casian Mabondo kwa nyakati tofauti wakiri wananchi kutoka vitongoji
sita walichangia nguvu ya mchanga,tofali kwa ajili ya upanuzi wa zahanati ya
awali na mradi mpya wa zahanati ya kisasa lakini walishangaa viongozi kuuza
kinyemela ilihali kuna kero ya ukosefu wa zahanati bora.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269