Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akimsikiliza kwa makini Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika
Berak wakati wa mazungumzo yao yaliofanyika ofisini kwake, Ikulu Jijini
Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe.
Malika Berak (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake,
Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba
alipomtembelea ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim
Lipumba mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake, Ikulu Jijini
Dar es Salaam jana.
...............................................................
Serikali
ya Ufaransa kupitia Benki ya Maendeleo ya Nchi hiyo (AFD) imeahidi kuwa
inampango wa kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu kutoka wastani
wa euro milioni 50 hadi euro milioni 100 kwa mwaka katika miaka ijayo
kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Balozi wa
Ufaransa hapa Nchini Malika Berak ametoa kauli hiyo Ikulu Jijini Dar es
Salaam alipokutana na Kufanya mazunguzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhusu hatua zilizofikiwa
katika uandaaji wa kongamano la uwekezaji litakalofanyika Jijini Dar es
Salaam kuanzia mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.
Balozi
huyo amesema mkopo huo itaiweza na kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo ya wananchi hasa katika sekta za maji na usafi
wa mazingira na miradi ya umeme.
Kuhusu
uandaaji wa kongamano la uwekezaji nchini, Balozi Malika Berak
amemweleza Makamu wa Rais kuwa maandalizi ya kongamano hilo kubwa la
Kibiashara linalolenga kujenga na Kuimarisha ushirikiano wa kibiashara
kati ya Tanzania na Ufaransa yanakwenda vizuri.
Balozi
huyo amesema kuwa kongamano hilo ambalo litakuwa la Kikanda litajadili
kwa kina fursa za uwekezaji hapa nchini hasa kwenye maeneo ya nishati,
usafirishaji, teknolojia ya habari na Mawasiliano na miradi ya
maendeleo.
Balozi
Malika Berak amemhakikishia Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kuwa
kongamano hilo la kibiashara litawakutanisha pamoja wafanyabiashara
Watanzania na wenzao wa Ufaransa katika kujadili na kubadilisha uzoefu
katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kibiashara kama hatua ya
kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.
Kwa
upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia
Suluhu Hassan ameipongeza Serikali ya Ufaransa kupitia kwa balozi wake
hapa nchi kwa ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika
sekta ya maji na usafi wa mazingira, nishati na mapambano dhidi ya
umaskini nchini.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Balozi wa Ufaransa hapa
nchini Malika Berat kuwa Tanzania itaendelea kudumisha na kuendeleza
mahusiano yaliyopo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande Mbili yaani
Tanzania na Ufaransa.
Makamu wa
Rais pia amepongeza jitihada za Serikali kupitia Ubalozi wake hapa
nchini za kuona umuhimu wa kuandaa Kongamano la kibiashara hapa nchini
ambalo litatoa fursa kubwa kwa watalaamu wa sekta mbalimbali nchini
kukutana na kujadiliana mambo kadhaa ikiwemo fursa za uwekezaji nchini.
Amesisitiza
kuwa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dakt John Magufuli inaendelea kuboresha mazingira
ya uwekezaji nchini kwa kupambana na vitendo vya rushwa kama hatua ya
kuhamasisha wawekezaji wengi kuja kuwekeza hapa nchini.Makamu wa Rais
amemweleza Balozi wa Ufarana hapa nchini kuwa milango ya ofisi yake ipo
wazi muda wote hivyo kama watakwama sehemu yeyote katika kuandaa
kongamano hilo amfahamishe haraka ili aweze kuchukua hatua haraka
kusaidia mchakato huo kutokana na muhimu wa kongamano hilo hasa wakati
huu ambapo Tanzania inataka kujenga uchumi wa viwanda nchini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269