RC
Makonda ameyasema hayo alipokuwa anafungua semina ya Walimu
wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) na kusisitiza kuwa viongozi wa
dini wakiwafundisha mema waumini ambao ndiyo wananchi Taifa halitakuwa
na wahalifu au matukio ya wizi, ujambazi, utumiaji wa dawa za kulevya na
ufanyaji wa biashara hiyo, jambo ambalo litaipunguzia gharama serikali
ya kuwahudumia waathirika kwa kuwapa vidonge vya Methadone, na serikali
haitatumia nguvu kubwa kujenga magereza kwa ajili ya wanaokiuka sheria
na taratibu za nchi.
Nakusisitiza kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono viongozi wa dini kwani wanamchango mkubwa kwenye maendeleo ya Taifa hili.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa JUWAQUTA ambaye pia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema kuwa lengo la semina hiyo ni
kuwaelimisha walimu hao juu ya kuunga mkono kauli mbiu ya HAPA KAZI TU ya
serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwani
kufanya kazi ni agizo kwa mujibu wa dini hiyo ya kiislamu ambapo waumini
wake wameambiwa wafanye kazi za halali ili wapate riziki halali na
siyo vinginevyo.
Huku
akifafanua kuwa hata manabii walikuwa wakifanya kazi hivyo ni vyema
kama viongozi kufuata nyayo hizo na kuwaamrisha wengine kufuata
utaratibu huo, pia Mwenyekiti huyo wa JUWAQUTA alitumia wasaa huo kwa
kujumuika na viongozi wengine kumuombea RC Makonda ili aendelee kutimiza
majukumu yake na Mwenyezi Mungu amlinde na mabaya.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269