Mohamed Abdullahi Farmajo
Waziri Mkuu wa zamani Mohamed Abdullahi Farmajo amechaguliwa kuwa
rais wa tisa wa Somalia. Aliteuliwa na Wambunge 184 kwa jumla ya wabunge
na wanaseneti waliokutana 328 chini ya ulinzi mkali katika jengo moja
la uwanja wa ndege wa Mogadishu siku ya Jumatano Februari 9.
Akiwa na umri wa miaka 54, Mohamed
Abdullahi Farmajo alikuwa Waziri Mkuu kuanzia mwezi Oktoba 2010 hadi
mwezi Juni 2011.Bw Farmajo anamrithi Hassan Sheikh Mohamoud ambaye
amempongeza. Uchaguzi wake umewashangaza wengi.
Anaitwa Mohamed Abdullahi Mohamed na
Wasomali wanamwita kwa jina maarufu "Farmajo". Mohamed Abdullahi Farmajo
ni maarufu nchini Somalia.
Rais huyo mpya wa Somalia, anatarajiwa kukabiliana na changamoto za kiuchumi, ugaidi, mivutano ya kisiasa kati ya koo mbalimbali na uhaba wa chakula katika nchi hiyo.
Rais huyo mpya wa Somalia, anatarajiwa kukabiliana na changamoto za kiuchumi, ugaidi, mivutano ya kisiasa kati ya koo mbalimbali na uhaba wa chakula katika nchi hiyo.
Uchumi wa taifa la Somalia, umeendelea
kuyumba hasa kwa sababu ya ukosefu wa uwekezaji na serikali kutumia
kiasi kikubwa cha fedha kidogo inachopata katika maswala ya usalama kwa
msaada wa nchi za nje.
Pamoja na hilo, ufisadi nchini humo
umesababisha uchumi kushuka kwa kiwango kikubwa kutokana na kupotea kwa
kiasi kikubwa cha fedha.
Ripoti ya mwaka uliopita iliyotolewa na
Shirika la Transparency International, ilieleza kuwa Somalia ndio nchi
inayoongoza kwa ufisadi duniani.
Sababu kubwa inayosababisha hili ni nchi hiyo iliyo kwenye eneo la pembe ya Afrika, kukosa taasisi za kukabiliana na tatizo hili.
Sababu kubwa inayosababisha hili ni nchi hiyo iliyo kwenye eneo la pembe ya Afrika, kukosa taasisi za kukabiliana na tatizo hili.
Uchaguzi wa wabunge uliofanyika mwaka
uliopita, uliripotiwa kukabiliwa pakubwa na utoaji rushwa,madai ambayo
pia yameripotiwa katika kampeni ya urais.
Pamoja na hilo, suala lingine ambalo
limeifanya Somalia kuendelea kuwa katika hali hii ni uwepo wa kundi la
kigaidi la Al Shabab.
Tangu mwaka 2006, kundi hili ambalo kwa
sasa linashirikiana na Islamic State, limeendeleza mashambulizi ya
kigaidi mjini Mogadishu kujaribu kuiangusha serikali inayotambuliwa
Kimataifa.
Kiongozi mpya atakuwa na kibarua cha
kuhakikisha kuwa kwa usaidizi wa jeshi la kulinda amani la Umoja wa
Afrika AMISOM, analimaliza kundi hilo ambalo linakadiriwa kuwa na
wafuasi kati ya 7,000 na 9,000 ndani na nje ya nchi.
Ugaidi nchini Somalia umesababisha maelfu ya raia wa nchi hiyo kukimbilia nchini Kenya na nchi zingine.
Framajo ni nani?
Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo alizaliwa 1962 mjini Mogadishu kutoka katika familia ya Gedo kusini magharibi mwa Somalia.
Mwaka 1985 alichaguliwa kuwa katibu wa kwanza katika ubalozi wa Washington DC.
Mwaka 1989, aliondoka na kujipatia shahada yake ya historia katika chuo kikuu cha Buffalo mjini New York .
Wakati huo Farmajo alitafuta hifadhi ya kisiasa nchini Marekani baada ya serikali ya Somalia kuanguka 1991.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269