Mahakama Kuu ya Kenya imebatilisha mpango uliotangazwa na serikali ya nchi hiyo wa kuifunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab.
Akitoa
hukumu hiyo leo, Jaji John Mativo amesema Waziri wa Usalama wa Ndani
Joseph Nkaissery na Katibu wake Mkuu Karanja Kibicho walichukua hatua
nje ya mamlaka yao kwa kuagiza kambi hiyo kubwa zaidi ya wakimbizi
duniani ifungwe.
Mahakama hiyo aidha imetangaza kuwa uamuzi wa kuwahamisha wakimbizi umekiuka Katiba na ni wa kibaguzi.
Mahakama
Kuu ya Kenya imetoa hukumu hiyo kufuatia shauri la madai
lililowasilishwa na Kamisheni ya Taifa ya Haki za Binadamu ya nchi hiyo
(KNCHR) na asasi ya Kituo cha Sheria.
Jaji
Mativo ameiagiza serikali ya Kenya iandae utaratibu utakaohakikisha
uhamishaji wa wakimbizi unafanyika kwa njia sahihi na mwafaka.
Kwa mujibu
wa hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama Kuu, notisi zilizochapishwa
kwenye gazeti kuu la serikali za kutangaza uhamishaji wa wakimbizi
zimeelezwa pia kuwa ni batili na zisizo na itibari.
Mwezi Mei mwaka uliopita wa 2006, Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya
Joseph Nkaissery, alitangaza kuwa ifikapo mwezi Novemba, serikali
itaifunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab kutokana na sababu za kiusalama,
kimazingira na kiuchumi pamoja na kuwatuhumu wafadhili wa kimataifa kuwa
hawachukui hatua za kutosha kuwasaidia wakimbizi hao.
Uamuzi huo
ulilaaniwa na kukosolewa vikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la
Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) pamoja na mashirika ya kutetea haki za
binadamu ya Human Rights Watch na Amnesty International.
Wakati
huohuo, masaa machache baada ya kutangazwa uamuzi huo wa Mahakama Kuu
hii leo, serikali ya Kenya kupitia msemaji wake Eric Keraithe imetangaza
kuwa sambamba na serikali hiyo ya muungano tawala wa Jubilee kuheshimu
sharia itakata rufaa kupinga hukumu hiyo…/
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269