Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akiwa amembeba mtoto huyo.
Jana mida ya saa 2 asubuhi katika maeneo
ya Stand kuu ya mabasi aliibiwa mtoto mchanga mweneye umri wa miezi 5.
Mtoto huyo aliibiwa na binti ambaye alikuwa amekuja kutafuta kazi.
Akieleza tukio hilo Mama yake Bi Asha
Shaban Lauza alisema ” nikiwa naosha vyombo binti huyu ambaye toka jana
alikuwa anatafuta kazi alianza kumpa maziwa mtoto yaliyo kwenye chupa
mpaka mtoto akamaliza , baadae mtoto akajinyea basi bila wasiwasi
nikampa shilingi elfu kumi ili akanunue pampasi duka la pili tu
akanyanyuka na mtoto kwenda dukani toaka asubuhi mpaka sasa usiku hatuja
muona” .
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh, Richard
Kasesela alifika eneo la tukio baada ya kumhoji mzazi akagundua
walichelewa kutoa taarifa polisi. Baada ya msako muda was saa 3 usiku
mtoto alipatikana eneo la Mkungugu km 33 kutoka Iringa Mjini.
Binti wa miaka 14 (Jina linahifadhiwa)
alikuwa akitoroka na mtoto huyo gari la polisi la doria likishirikiana na
wananchi wa kijiji cha Mkungugu lilifanikiwa kumuweka chini ya ulinzi
mwizi huyo wa mtoto. Mkuu wa Wilaya alifika akiongozana na mama Mzazi wa
mtoto pamoja na Diwani wa kata ya Kisinga Mh, Ritha Mlagala.
Binti mwizi yupo kituo cha polisi
akiendelea kuhojiwa na mama mzazi baada ya kuandika maelezo alipewa fomu
ya matibabu na kumpeleka mtoto hospitali.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh, Richard
Kasesela amekemea vikali kitendo cha uzembe wa mama huyu na wazazi kwa
ujumla “pamoja na mama huyu kuwa na uchungu wa mtoto bado ana mashtaka
ya kujibu ya uzembe, watu tusio wajua tusiwape watoto wetu hata kidogo
huu ni uzembe wa hali ya juu” alisisitiza
Mkuu wa wilaya. Pichani anaonekana mtoto
Latifa akiwa ambebwa na Mkuu wa wilaya walipofika kituo cha polisi.
Picha zingine ni za eneo la kijiji cha Mkungugu barabani alipokamatwa
binti mwizi akiwa na mtoto usiku wa saa 3.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269