Yule anaeaminika kuwa mwanamke mnene kabisa duniani
amewasili nchini India kwa ajili ya upuasuaji wenye lengo la kupunguza
uzito wake.
Madaktari wameanza maandalizi ya kumfanyia upasuaji wa dharura kwa
kumnywisha kimiminika kitakachomwezesha kupunguza uzito. Hatua hiyo
inatokana na waziri wa mambo ya nje kuingilia na kutoa ahadi ya
kufanikisha upatikanaji wa visa kwa ajili ya safari hiyo. Eman Ahmed Abd
El Aty, mwenye umri wa miaka 36, anakadiriwa kuwa na kilo 500. Kutokana
na umbo lake amesafiri katika nafasi maalumu ya ndege iliyotengenezwa
kwa ajili yake. Hivi karibuni dada wa bonge huyo, alimwendea dokta
Lakdawala na kumweleza kuwa ndugu yake anahitaji huduma ya dharura ya
matibabu. Alikuwa anavimba viungo vyake na kuandamwa na maradhi mengine
ya moyo na sukari. Safari ya Eman imekuwa changamoto kubwa na hasa kwa
kuzingatia umbile lake lililomfanya hasindwe kujongea au kutembea na
kusalia ndani ya nyumba kwa zaidi ya miaka 25 sasa. Wachunguzi wa mambo
wanasema kama uzito wa Abd El Aty utathibitika basi atakuwa kavunja
rekodi iliyowekwa na Pauline Potter wa Marekani ambae alikuwa na uzito
wa pauni 643, na kufanya awe na rekodi ya mwanamke mwenye uzito wa juu
kabisa aliye hai. India imekuwa kivutio kikubwa kwa kutoa tiba bora na
nafuu ikilinganishwa na mataifa ya Magharibi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269