Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ameitaka nchi ya Uingereza
kutazama uwezekano wa kufanya biashara na Tanzania kwa kununua bidhaa
zilizoongezwa thamani badala ya hali ya sasa ambapo nchi hiyo imekuwa
ikinunua bidhaa ghafi ilihali ikiingiza nchini bidhaa zake za viwandani.
Dkt.
Mpango ameyasema hayo alipokutana na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza
anayeshughulikia masuala ya Biashara Bw. Lord Hollick ailipo tembelea
Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
Amesema
Tanzania inataka kuona inauza bidhaa zake zenye thamani ambazo
zitatokana na maendeleo makubwa ya viwanda hapa nchini ikiwa ni Sera ya
nchi kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025.
Nchi
ya Uingereza imekuwa ikifanya biashara na Tanzania kwa kiasi kikubwa na
takwimu zinaonesha nchi hiyo inaingiza bidhaa zenye thamani mara nane ya
Tanzania jambo ambalo linatakiwa kurekebishwa ili biashara iwe na
manufaa kwa pande zote mbili.
Miongoni
mwa bidhaa ghafi ambazo zimekuwa zikisafirishwa kwenda uingereza ni
pamoja na Chai, kahawa na madini ya vito huku Uingereza ikiingiza bidhaa
za viwandani zenye thamani kubwa ikijumuisha mashine (mitambo),vifaa
vya umeme, bidhaa za plastiki na madawa.
Kwa
upande wake, Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia
Biashara Bw. Lord Hollick amebainisha nia ya nchi yake kutaka kuwekeza
kwa kiasi kikubwa katika nchi za Afrika ikiwemo Tanzania baada ya Taifa
hilo kuamua kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.
Maeneo
ambayo Uingereza inapenda kuwekeza Tanzania ni katika Sekta ya Kilimo,
Nishati ya Umeme na Usafirishaji huku kwa sasa akionesha nia ya ya nchi
yake kuwekeza katika ujenzi wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Msalato katika Makao Makuu ya nchi - Dodoma.
Pia
nchi hizo mbili zimekubaliana kuandaa mkutano utakao wakutanisha
Serikali na Sekta Binafsi ya Tanzania kwa upande mmoja na wawekezaji
wakubwa kutoka Uingereza na nchi nyingine za Ulaya ambao utasaidia
kukuza uwekezaji na biashara na kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi
kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na nchi hizo za Ulaya ikiwemo
Uingereza.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akieleza
kuhusu juhudi za Serikali katika kutengeneza mazingira mazuri ya
kibiashara wakati wa mkutano na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza
anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick katika ukumbi wa Wizara hiyo
jijini Dar es salaam.
Wajumbe
wa Mkutano walioongozana na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza
anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick, wakisikiliza kwa makini
maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb)
(hayupo pichani), kuhusu umuhimu wa kufanya biashara ya bidhaa
zilizoongezwa thamani ili kukuza viwanda vya ndani, wakati wa mkutano
huo jijini Dr es salaam.
Mjumbe
wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick
(kushoto) akifafanua jambo wakati wa Mkutano kati yake na Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani) kuhusu
nia ya kuwekeza katika ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Msalato Dodoma,
Kulia ni Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke, Mkutano
uliofanyika Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es salaam.
Mjumbe
wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick
(kulia) akisisitiza kuhusu kuendelea kuimalisha uhusiano wa kibiashara
kati ya Tanzania na Uingereza huku Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb) (kushoto) akimsikiliza kwa makini katika ukumbi wa
Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akipeana
mkono na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara
Bw. Lord Hollick (kulia) baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao kuhusu
Mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili, uliofanyika katika
ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
Wajumbe
wa Mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb)
na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord
Hollick wakisalimiana baada ya kumalizika kwa mkutano huo na kuazimia
pamoja na mambo mengine, kufanyika kwa Mkutano utakaowakutanisha
wawekezaji wakubwa wa nchi hizo mbili, Mkutano uliofanyika katika ukumbi
wa Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269