Breaking News

Your Ad Spot

Feb 17, 2017

WASI WASI WA JAMII YA KIMATAIFA KUHUSU MCHAKATO WA KISIASA DRC

Jamii ya kimataifa imebainisha wasiwasi wake kuhusu kuwepo mkwamo katika mazungumzo ya kuhitimisha mgogoro wa kisiasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Katika taarifa ya pamoja jumuiya za kimataifa zikiwemo Umoja wa Afrika AU, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya EU na Jumuiya ya Kimataifa  ya Nchi Zinazozungumza  Kifaransa IOF zimesema zinahofu kuhusu kuendelea kwa mkwamo kwenye mjadiliano ya kisiasa miongoni mwa wadau nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuhusiana na utekelezaji wa  makubaliano ya kisiasa yaliyoafikiwa Desemba 31 mwaka jana. 
Mashirika hayo manne yamesema yamebaini kwamba wiki sita baada ya makubaliano ya kipindi cha mpito ili kuelekea kufanya uchaguzi huru wa amani na haki Desemba 2017, pande husika bado hazijakamilisha majadiliano ya utekelezaji wa mkataba.
Maandamano ya wapinzani DRC
Yameongeza kuwa hali hiyo inaweza kutia dosari nia njema iliyopelekea kutiwa saini makubaliano mwezi Desemba mwaka jana.
Hivyo mashirika hayo yametoa wito kwa wadau wote nchini DRC ikiwa ni pamoja na upande wa serikali na wapinzani kuongeza maradufu juhudi kwa nia njema ili kuharakisha na kukamilisha majadiliano yanayoendelea, kwani wamesema kuna haja ya pande zote kushikamana katika mchakato wa upatanishi na kuhakikisha makubaliano ya 31 Desemba yanatekelezwa kwani ni muhimu sana kabla ya uchaguzi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages