Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyaka na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (kulia) akiongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa hospitali hiyo Dar es Salaam leo
Baadhi ya Wajumbe na Wafanyakazi wa hospitali hiyo wakimsikiliza mwenyekiti wa baraza hilo leo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa hospitali hiyo wakimsikiliza mwenyekiti wa baraza hilo leo.
Ofisa Masoko wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), Margerate Mrina akitoa mada kwenye mkutano wa Baraza la wafanyakazi ambao umefanyika leo. |
Mkurugenzi
wa Fedha na Mipango wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Gerald
Jeremiah akiuliza swali kwenye mkutano huo leo. Kutoka kushoto ni
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika hospitali hiyo, Dk. Hedwiga Swai,
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk. Julieth Magandi, Mkuu wa Idara ya
Watoto, Dk. Mary Charles na Mkuu wa Idara ya TEHAMA, Patrick Muro
wakifuatilia mkutano huo leo.
Mwakilishi wa Idara ya Tiba katika hospitali hiyo, Dk. Primus Saidia akiuliza swali katika mkutano huo leo.
Wafanyakazi wa hospitali hiyo na baadhi ya wajumbe
Mkurugenzi Msaidizi- Elimu na Ushirikishwaji, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Andrew Mwalwisi akitoa mada leo
kwenye mkutano huo leo.
Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo limekutana katika kikao cha 17 pamoja na mambo mengine wajumbe wa baraza hilo wametakiwa kutoa maoni na michango kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma kwenye hospitali hiyo.
Akitoa mada katika kikao hicho Mkurugenzi msaidizi –Elimu na ushirkishwaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Andrew Mwalwisi amewataka wajumbe wa baraza hilo kuhakikisha wanatoa mrejesho wa vikao vya baraza kwa wafanyakazi kwa sababu yanayojadiliwa ni kwa maslahi ya watumishi wote wa Muhimbili.
“Wale wenzenu mkawaeleze tunayoyazungumza hapa, hivyo ni vizuri mkawaeleze michango mbalimbali inayotolewa kwenye mkutano huu kwani na wenyewe wanatakiwa kufahamu ambacho kimejadiliwa katika kikao hiki,” amesema Mwalwisi.
Agenda zilizopokelewa na kujadiliwa ni mafanikio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2015/16 na robo mwaka 2016/2017. Pia, Baraza limepokea na kujadili makadirio ya bajeti ya mwaka fedha 2017/2018.
Kabla ya kuanza kwa kikao cha baraza la wafanyakazi, wajumbe wamemchagua Eneza Somolon Msuya kuwa katibu wa baraza hilo, huku Merina Rwechungura akiwa Katibu Msaidizi.

No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269