baadhi
ya wananchi wakichukuliwa vipimo vya afya na madaktari kutoka kcmc
pamoja na Mounti meru Hospital ikiwa ni huduma inayotolewa bure katika
viwanja vya kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid katika wiki ya wanawake
duniani ambayo kwa mkoa wa Arusha imeandaliwa na Phide intantament
baadhi
ya wananchi wakiwa katika mstari wakisubiri kuchukuliwa vipimo vya
magonjwa mbalimbali bure yakiwemo ,Kisukari ,Presha,Kansa ,Ukimwi na
mengineyo
mmoja wa madaktari akiendelea kupima mara baada ya kuchukuwa vipimo vya wagonjwa ndani viwanja vya Sheikh Amri Abeid
Na Woinde Shizza,Arusha
Maadhimisho
ya wiki ya wanawake duniani yameanza rasmi mkoani Arusha ambapo
wananchi wa mkoa wa Arusha pamoja na vitongoji vyake wamepata fursa ya
kupata huduma ya kupima magonjwa mbalimbali bure
zoezi
hilo ambalo limeanza leo jijini hapa katika kiwanja cha sheikh Amri
Abeid limeonekana kuwavuta wananchi wengi kwani zaidi ya wananchi 100
wamejotokeza kupima afya zao bure katika viwanja hivyo
Akiongea
na waandishi wa habari muandaaji wa maathimisho hayo ya wiki ya
wananwake duniani kwa mkoa wa Arusha mkurugenzi wa Phide Intantament
Phidesia Mwakitalima alisem akuwa muamko ni mzuri na wananchi wameanza
kujitokeza kwa wingi
Alisema kuwa pamoja ni siku ya kwanza tu lakini zaidi ya wananchi 100 wamejitokeza kupima afya zao hivyo ni jambo zuri mno
Alisema
kumekuwepo na tabia ya wananchi wengi kutokuwa na tabia ya kupima afya
zao hadi pale wanapoumwa kitu ambacho sio kizuri na kuwataka wananchi
kujijengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara
Zoezi
hili la kupima afya limeanza leo na linatarajiwa kumalizika march nane
na huduma za kupima magonjwa mbalimbali na ushauri wa aina mbalimbali
ikiwa ni pamoja na watu kuchangia damu unatolew bure hivyo ni wajibu wa
kila mwananchi kutumia fursa hiii ili kujua afya yake
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269