Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga,
Albert Msovela akizungumza na madaktari wa Kinywa na Meno kutoka sehemu
mbalimbali wakiwemo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es
Salaam (pichani hawapo) wakati walipofika Ofisini kwake na
kujitambulisha katika kuelekea Maadhimisho ya siku ya Wiki ya Kinywa na
Mane ambapo kilele ni machi 20, Dodoma na anatarajiwa mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana, ambapo Katibu Tawala
huyo alisema, napenda kutowa shukrani za kipekee na kwaniaba ya Mkoa
wangu kwa jinsi mnavyo jitowa katika kuwahudumia ndugu zetu, watoto
wetu na mgeweza kwenda sehemu nyingine lakini kwa mfululizo wa miaka
mitatu mnakuja kututembelea na kutowa huduma, misaada na elimu ya jinsi
ya kutunza afya ya kinywa na meno na sasa kunamabadiliko makubwa tofauti
na mara yakwanza mlipofika na baada ya hapo wengi walijitokeka katika
kusaidia watoto hao, nawaombea kwa Mungu mpate kuja kututembelea kwa
mara nyingine, karibuni sana hapa ni kwenu na msisite kuniona na pia
nitafika kuja kuwaona kabla hamjafunga huduma hiyo. hayo aliyasema leo
ofisini kwake baada ya kutembelewa na Madaktari wa afya ya meno
walipomtembelea ofisini kwake katika kuelekea Maadhimisho ya wiki ya
kinywa na meno. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Madaktari wa Kinywa na Meno wakikaribishwa na watoto wa Shule ya Msingi Buhangija Mkoani Shinyanga kwa wimbo
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Jumuishi ya Kata ya Buhangija Mkoani Shinyanga wakifurahia jambo |
Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno
Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salamu, Conrad Mselle akitowa Elimu
ya upigaji mswaki wa Kinywa na Meno leo mbele ya wanafunzi wa shule hiyo
katika kuelekea kilele cha Maadhimisho yatakayofanyika machi 20, mwaka
huu Dodoma, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa, Jordan
Rugimbana
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania, Dr. Lorna Carneiro akizungumza na wanafunzi hao
Daktari wa Meno Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya akifungua wiki ya kinywa na Meno leo katika Shule ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Jumuishi ya Kata ya Buhangija Mkoani Shinyanga
Maktari Bingwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili, Habiba Madjapa (kulia) na Dr Arnold Mtenga (katikati)
wakijadiliana na Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno, Tanzania
Dr. Lorna Carneiro (kushoto)
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na madaktari hao
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (kulia ) akikabidhiwa flana na Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania, Dr. Lorna Carneiro mara walipofika na msafara wake kwa lengo la kujitambulisha
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno, Tanzania Dr Lorna Carneiro (kushoto) akizngumza jambo wakati walipofika yeye na msafara wake kumsalimia Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (kulia) katikati ni Daktari wa Meno Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (katikati aliyevaa koti) akizungumza na madaktari hao (kulia )
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269