Habari kutoka mkoa wa Nainawa (Nineveh)
nchini Iraq zinaarifu kwamba jeshi la nchi hiyo limedhibiti jengo la
redio ya kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh kwa jina la al-Bayan.
Jeshi la Iraq limekomboa eneo la Jawasaq katika pwani ya upande
wa kulia ya mji wa Mosul, sambamba na kubaini jengo na mnara wa
kurushia matangazo wa redio ya kundi hilo kwa jina la al-Bayan katika
mji huo. Kabla ya jeshi la Iraq kuwasili katika eneo hilo, genge hilo la
kigaidi lililichoma moto jengo la redio hiyo ili kupoteza ushahidi.
Hata hivyo jeshi la Iraq liliweza kunasa nyaraka muhimu katika nyumba
iliyokuwa karibu na jengo la redio hiyo ambazo zinajumuisha ripoti
muhimu za kiintelijensia za timu yote ya kundi hilo.
Itafahamika kuwa, redio hiyo ya kundi la Daesh (ISIS) ilikuwa
ikitangaza kwa lugha tano tofauti na kutoa matangazo ya kuwataka raia
kutekeleza operesheni za kigaidi. Kusambaratishwa redio hiyo kunatajwa
kuwa pigo jingine kubwa dhidi ya genge hilo linalopata himaya kutoka
Marekani, Israel, Saudia na baadhi ya za Kiarabu na Magharibi.
Wakati huo huo kitengo cha intelijensia katika jeshi la Iraq
kimetangaza habari ya kuuawa Abu Abdur-Rahman al-Answar, kiongozi wa
genge la kigaidi kwa jina la Jundul-Khilafah lenye mafungamano na kundi
la Daesh huko magharibi mwa mji wa Mosul. Kwa mujibu wa ripoti hiyo
gaidi huyo mwenye uraia wa Saudia ameuawa katika shambulio la anga akiwa
pamoja na viongozi wengine sita wa kundi hilo.
Jeshi la Iraq lilmetanga kuwa, kundi la Daesh (ISIS) limekuwa
likitumia silaha zenye gesi ya sumu katika kulizuia jeshi hilo kusonga
mbele katika maeneo yaliyosalia ya mji huo wa Mosul.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269