Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa
Mataifa limetahadharisha kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu
unaofanyika katika nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya
Uajemi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutteres ambaye
amehutubia kikao cha 34 baraza hilo mjini Geneva amekosoa vikali
ukiukwaji wa haki za binadamu katika nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi
na kutahadharisha kuhusu upuuzwaji wa haki za binadamu. Baraza la
Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi linaundwa na nchi za Saudi Arabia,
Kuwait, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu, Oman na Bahrain.
Vilevile mwakilishi wa Uholanzi katika Baraza la Haki za Binadamu la
Umoja wa Mataifa amezikosoa nchi zinazopuuza mchango na nafasi ya
watetezi wa haki za binadamu katika nchi za Kiarabu hususan Bahrain na
kutoa wito wa kuwepo ushirikiano katika uwanja huo.
Wakati huo huo taasisi na jumuiya za kutetea haki za binadamu
likiwemo shirika la Human Rights Watch zimezitaka nchi wanachama na
watazamaji katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kutoa
taarifa ya pamoja kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu
unaofanyika nchini Bahrain. Vilevile yametoa wito wa kuboreshwa haki za
binadamu nchini humo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269