Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
limeufanyia majaribio mfumo wa makombora wa S 300 wa Iran kwa operesheni
iliyofanikiwa katika jangwa la katikati mwa nchi.
Majaribio ya mfumo huo yamefanyika
leo kwa lengo la kuchunguza uwezo wa utendajikazi wake na yameenda
sambamba na kumefyatuliwa makombora tofauti yakiwemo ya balestiki na
ndege zisizokuwa na rubani.
Brigedia Jenerali Farzad Esmaili,
kamanda wa kituo cha Jeshi la Anga cha Khatamul-Anbiyaa katika jeshi la
Iran ameliambia Shirika la Habari la IRNA kwamba, mfumo wa
S-300 umeunganishwa na mifumo mingine ya ulinzi yenye uwezo ya taifa
hili kama vile 'Mirsad" na "Talash' ili kulinda anga ya Iran.
Brigedia Jenerali Farzad Esmaili, amesisitiza kuwa jibu la bwabwaja
za adui wa Iran ya Kiislamu litaonekana katika medani za vita na
kuongeza kuwa, wataalamu wa Iran wameufanyia majaribio mfumo huo kwa
msingi wa vitisho vya adui na kwamba hakuna mtu mwingine anayeweza
kufahamu utendajikazi wa mfumo huo.
Brigedia Jenerali Esmaili amesema kuwa, mbali na mfumo wa S-300,
jeshi la Iran hivi karibuni litaufanyia majaribio mfumo wa Bavar 373 wa
nchi hii ambao unashabihiana na ule wa S-300. Amesema kuwa, mfumo wa
S-300 wa Iran ni wa kisasa zaidi ukilinganishwa na ule wa S-300 wa
Russia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269