Mkuu
wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla
(kulia), akizungumza Makao Makuu ya Kampuni hiyo Barabara ya Nyerere
jijini Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya kuwaaga vijana wanne wa
kitanzania ambao wanakwenda nchini India kwa mafunzo ya miezi tisa ya
kutengeneza magari. Kutoka kushoto ni viongozi wa kampuni hiyo, Sarvan
Keshri na Udayagiri Veeru.
Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla (kulia), akisisitiza jambo.
Mgeni
rasmi katika hafla fupi ya kuwaaga vijana hao Mkurugenzi Msaidizi
Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu,
Robert Masatu Masingi akizungumza katika hafla hiyo. Kutoka kushoto ni mmoja wa viongozi wa kampuni ya Tata, Udayagiri Veeru na Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla.
Viongozi wa kampuni hiyo ukitoa zawadi ya ua kwa mgeni rasmi Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masatu Masingi.
Viongozi wa kampuni hiyo mgeni rasmi, wazazi na ndugu wa vijana hao wakiwa katika picha ya pamoja.
Mgeni
rasmi katika hafla fupi ya kuwaaga vijana hao Mkurugenzi Msaidizi
Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu,
Robert Masatu Masingi (kulia), akikabidhiwa zawadi ya picha ya tembo na
viongozi wa kampuni hiyo. Kutoka kushoto ni Udayagiri Veeru na Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla.
Mama
wa msichana pekee anayekwenda kupata mafunzo hayo, Fatma Mussa
Ngulangwa (kushoto), akimkabidhi binti yake, Mariam Shamte maua ikiwa ni
ishara ya kumuaga.
Fr.Lucas Wakuganda akimkabishi maua mtoto wake anayeondoka kwenda masomoni nchini humo.
Mhitimu wa mafunzo hayo, Osmund Kapinga (katikati), akiwa amewainua mikono vijana hao ikiwa ishara ya kuwaaga.
Mkufunzi
wa mafunzo wa kampuni hiyo, Oscar Mwakagenda (kushoto), akitoa
maelekezo ya injini za gari zinazofanya kazi mbele ya mgeni rasmi na
uongozi wa kampuni hiyo.
Ni furaha tupu katika hafla hiyo.
Viongozi wa kampuni hiyo mgeni rasmi, wazazi na ndugu wa vijana hao wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya karakana ya mafunzo. |
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Tata imetoa ufadhili kwa vijana wanne wa kitanzania kwenda nchini India kujifunza utengenezaji wa magari.
Kati
ya vijana hao msichana ni mmoja ambapo wanatarajia kuondoka nchini
kesho kuelekea mji wa Jamshedpur nchini humo kwa mafunzo ya miezi tisa
kupitia mpango wa Skill pro- International Business Commarcial Vehicles
Skill Development Program.
Mgeni
rasmi katika hafla fupi ya kuwaaga vijana hao Mkurugenzi Msaidizi
Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu,
Robert Masatu Masingi akizungumza Dar e Salaam jana aliwataka vijana
hao wakiwa nchini humo kuwa mabalozi wa kutangaza sifa nzuri ya Tanzania
na si vinginevyo.
"Tumieni
fursa hii mliyoipata kwenda kusoma na kuitangaza nchi yetu msiende
kucheza na kututia aibu kwani katika vijana 25 kutoka nchi mbalimbali za
Afrika nyie wanne ndio mnaiwakilisha nchi yetu" alisema Masingi.
Masingi
aliishukuru kampuni hiyo kwa kuwawezesha vijana hao na kuahadi serikali
kushirikiana nayo ili kupanua soko la ajira kwa vijana nchini.
Mkuu
wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania Prashant Shukla
alisema hii ni awamu ya tatu kwa kampuni hiyo kupeleka vijana nchini
India kujifunza kutengeneza magari ambapo kwa awamu ya kwanza hakuna
kijana wa kitanzania aliyehudhuria mafunzo hayo.
Alisema
kwa awamu ya pili alipelekwa mtanzania Osmund Kapinga ambaye aliibuka
kuwa mwanafunzi bora na katika awamu hii ya tatu wanakwenda hao wanne.
Alisema
lengo la kuwapeleka vijana hao nchini India ni kujifunza kazi hiyo ili
nao wakirudi waweze kuwa walimu wa wenzao hivyo kuisaidia serikali
kukuza ajira nchini hasa kwa vijana.
Alisema
kampuni hiyo kwa Tanzania inafanya kazi mikoa ya Dar es Salaam, Arusha
na Mwanza lakini wanatarajia kwenda mkoani Mbeya kufungua tawi na
baadae itafuatia mikoa mingine ambapo vijana wanaopata mafunzo kupitia
mpango huo wataenda kuwafundisha wenzao.
Mhitimu
wa mafunzo hayo nchini humo Osmund Kapinga alisema kampuni hiyo ni
kubwa na mbali ya kutengeneza magari ya aina zote inavitu vingi inavyo
tengeneza hivyo aliwasihi wenzake wanaoondoka kuchangamkia fursa hiyo
hadimu ili wakirudi waweze kuwasaidia watanzania wenzao.
Vijana
waliopata fursa ya kwenda kupata mafunzo hayo ni Mariam Hemed Shamte,
Anord Peter Nditu, Elias Jones Tette na Adam Abdallah Pwimu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269