Na Magreth
Magosso,Kigoma
WATOTO Yatima na waishio katika mazingira magumu
wanaofadhiliwa na Kanisa la Africa, Inland (AIC) Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na Shirika la
Compassion wametoa zawadi ya misa maalum ya kutoa shukrani kwa wahisani hao kwa
kuonyesha vipaji mbalimbali ambavyo wamefundishwa na walezi wa kanisa hilo kituo
cha 973 mkoani hapa kwa kipindi cha
zaidi ya Miaka mitatu.
Wakizungumza na Jambo Leo
jana baada ya misa hiyo Baadhi ya watoto hao akiwemo Paulo Obed na Aziz
Ally kwa nyakati tofauti walisema wanawaombea mungu wahisani hao ambao wamewapa
mwanga wa kutimiza ndoto zao za kielimu kwa kuwapa huduma za msingi hasa mahitaji
yote ya kielimu na afya pindi wanaposhikwa na maradhi.
Walisema mbali hilo wanahudumiwa
chakula ,mavazi na kuwakumbusha walezi na wazazi wasiepuke majukumu yao katika
kutoa malezi ya kumcha mungu kwa watoto yatima na waishio katika mazingira
hatarishi ambao chimbuko kubwa ni walezi kukwepa majukumu yao.
Walisema kupitia misa
hiyo wamebaini vipaji vyao vya uimbaji,ujasiri wa kusimama mbele ya watu wengi
na kutoa neno la mungu sanjari na kuwa viongozi wa taifa hilo siku za usoni na
kutoa mwito kwa watoto wenzao watumie akili katika kujikwamua na changamoto
zinazowakabili na wasitumie vibaya miili yao katika vitendo viovu.
Kwa upande wa walezi wa
watoto hao Elizabeth Nyanda alisema wanalea watoto kuanzia umri wa miaka mitatu
na kuendela ambao ni yatima na wenye mazingira magumu kutoka familia tofauti
tofauti na wanawapa elimu kuu Nne ambazo
ni elimu ya kiroho,kimwili,kijamii ambapo yanampa ujasiri wa kujitegemea kwa
kumtanguliza mungu ambaye ndio mwisho la hitaji la wanadamu wema.
Naye Mkurugenzi wa Kituo
hicho Robert Chamungu alisema kituo kinapokea watoto yatima na waishio katika
mazingira magumu bila kujali tofauti za udini kwa lengo la kuendelea ndoto zao
siku za usoni hali inayochangia wahisani kutoka Compassion na kanisa kutoa
huduma za elimu na afya kwa walengwa.
Alisema changamoto
kubwa ni baadhi ya mashirika ya kuhudumia watoto kutokushirikiana kwa dhati
katika kumkwamua mtoto mwenye hitaji la msingi na kushauri wadau wa watoto wa
aina hiyo washirikiane katika kuimarisha ndoto za watoto katika huduma za msingi,hasa
alimu,afya,chakula,makazi na mavazi na si kunyang`anyana watoto kwa kutoa
huduma zinazofanana.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269